May 10, 2018

Kipa namba moja wa Yanga, Mcameroon Youthe Rostand ameshindwa kusafiri na kikosi cha timu yake jana kuelekea Mbeya kwa ajili ya mchezo wa ligi dhidi ya Tanzania Prisons.

Rostand ameungana na baadhi ya wachezaji wa Yanga waliosalia Dar es Salaam ikielezwa wanadai fedha zao za malipo ya mishahara.

Kipa huyo ambaye ni tegemeo kwa Yanga ameshindwa kuungana na wenzake katika safari ya Mbeya ambapo leo ina kibarua dhidi ya Tanzania Prisosons kwenye Uwanja wa Sokoine jijini humo.

Beno Kakolanya ambaye hajacheza kwa muda mrefu atachukua nafasi ya Mcameroon huyo leo langoni.

Mbali na Kooanya kutosafiri na timu, Ramadhani Kabwili yeye ameungana na kikosi cha timu ya Taifa ya vijana, Ngorongoro Heroes kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa kuwania kucheza AFCON (U20) dhidi ya Mali.

4 COMMENTS:

  1. Haya ndiyo maandalizi dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda. Kwa nini viongozi wa Yanga haui wakweli juu ya masuala magumu kama haya? Mamilioni ya CAF yanafanya nini sasa, kwa nini msikope na kisha fedha za CAF zikija mnarudisha ili kuleta upinzani mchezoni?

    ReplyDelete
  2. Kakolanya ndo best keeper kwa Yeboyebo. Huyo mcameroon ni shati tu. Ana makosa kibao yanayoathiri timu

    ReplyDelete
  3. Mi ni mmoja ya washabiki ninaoungana na wachezaji katika suala lao la kugomea michezo kwa kushinikiza kupewa kwa malipo ya fedha zao. Viongozi wa Yanga wameshindwa katika neno linaloitwa "Uwazi"...maana hata ukiwa muwajibikaji kiukweli lakin ukafeli kuwa muwazi wa mambo ya timu itakuwa umekosea sana. Yanga inafeli kutokana na viongozi kutoweka mambo hadharani. Kuna watu wana nia ya kusaidia lakini wanashindwa kutokana na sentensi za akina ten na Mkwasa kwamba timu haina tatizo.

    Nafikili wanachama wafanye shinikizo kwa uongozi kuitisha mkutano wa dharura wa wanachama ili kujaribu kuzungumza masuala kadhaa. Moja ya kitu ninachojiuliza ni kwamba hizi fedha za wadhamini zimetumika wapi.???wapi fedha za mgawo wa mlangoni??.

    Timu ina wadhamini wasiopungua wanne ambao ni:--
    1) Vodacom Tanzania
    2) Macron
    3) Maji ya Afya
    4) Sportpesa
    5) Azam Production kupitia Azam TV

    Nafikili ni muda wa viongozi kuja kutusomea taarifa ya mapato na matumizi na kama kuna tatizo lazima wachukuliwe hatua.Lazima viongozi watoe taarifa kuhusu matumizi ya Fedha za Sportpesa ambazo ni zaidi ya Bilioni moja, Azam Tv ambazo ni zaidi ya milion mia, Macron (hazijajulikana) na Vodacom tanzania.

    NB: Kama viongozi ni watu wenye nia njema isingeshindikana kuwalipa wachezaji mishahara hata siku moja. Yanga au Simba ni Taasisi na si timu ya mtu..kiongozi mmoja akitoka au akimaliza muda wake mwngine anaingia. Yanga au Simba haziwezi kushindwa kuchukua pesa kwenye Taasisi za Kifedha. Tunapata tatizo kwa kuwa viongozi wengi wa Timu zetu wapo kimaslahi zaidi hawawazi kuhusu maendeleo ya timu.

    Yanga imeshindwa kujua tatizo lake ni lipi zaidi ya kupambana na wachezaji wanaogoma. Leo tunamuona Beno ndio muokozi wetu wakati tulianza kumtupa. Sasa unajiuliza "Mmemleta kocha aone matatizo au afundishe Timu..?" maana sioni anachofanya zaidi ya kuona matatizo ya timu. Tulitakiwa kwanza tutatue matatizo yetu ya ndani ndio aletwe kocha. Sasa nini maana ya hii kitu?

    ReplyDelete
  4. Mi ni mmoja ya washabiki ninaoungana na wachezaji katika suala lao la kugomea michezo kwa kushinikiza kupewa kwa malipo ya fedha zao. Viongozi wa Yanga wameshindwa katika neno linaloitwa "Uwazi"...maana hata ukiwa muwajibikaji kiukweli lakin ukafeli kuwa muwazi wa mambo ya timu itakuwa umekosea sana. Yanga inafeli kutokana na viongozi kutoweka mambo hadharani. Kuna watu wana nia ya kusaidia lakini wanashindwa kutokana na sentensi za akina ten na Mkwasa kwamba timu haina tatizo.

    Nafikili wanachama wafanye shinikizo kwa uongozi kuitisha mkutano wa dharura wa wanachama ili kujaribu kuzungumza masuala kadhaa. Moja ya kitu ninachojiuliza ni kwamba hizi fedha za wadhamini zimetumika wapi.???wapi fedha za mgawo wa mlangoni??.

    Timu ina wadhamini wasiopungua wanne ambao ni:--
    1) Vodacom Tanzania
    2) Macron
    3) Maji ya Afya
    4) Sportpesa
    5) Azam Production kupitia Azam TV

    Nafikili ni muda wa viongozi kuja kutusomea taarifa ya mapato na matumizi na kama kuna tatizo lazima wachukuliwe hatua.Lazima viongozi watoe taarifa kuhusu matumizi ya Fedha za Sportpesa ambazo ni zaidi ya Bilioni moja, Azam Tv ambazo ni zaidi ya milion mia, Macron (hazijajulikana) na Vodacom tanzania.

    NB: Kama viongozi ni watu wenye nia njema isingeshindikana kuwalipa wachezaji mishahara hata siku moja. Yanga au Simba ni Taasisi na si timu ya mtu..kiongozi mmoja akitoka au akimaliza muda wake mwngine anaingia. Yanga au Simba haziwezi kushindwa kuchukua pesa kwenye Taasisi za Kifedha. Tunapata tatizo kwa kuwa viongozi wengi wa Timu zetu wapo kimaslahi zaidi hawawazi kuhusu maendeleo ya timu.

    Yanga imeshindwa kujua tatizo lake ni lipi zaidi ya kupambana na wachezaji wanaogoma. Leo tunamuona Beno ndio muokozi wetu wakati tulianza kumtupa. Sasa unajiuliza "Mmemleta kocha aone matatizo au afundishe Timu..?" maana sioni anachofanya zaidi ya kuona matatizo ya timu. Tulitakiwa kwanza tutatue matatizo yetu ya ndani ndio aletwe kocha. Sasa nini maana ya hii kitu?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic