YANGA KUIVAA PRISONS LEO IKIWA NA WACHEZAJI PUNGUFU
Kikosi cha Yanga kinateremka dimbani Sokoine jioni ya leo kuvaana na Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Uongozi wa Yanga umesema unataka kutengeneza heshima hata kama wataukosa ubingwa wa ligi kwa kushinda mechi zote zilizosalia.
Yanga inashuka dimbani ikiwa pungufu kufuatia nyota wake kadhaa kusalia jijini Dar es Salaam ikilelezwa kuwa ni madai ya mshahara.
Msafara wa Yanga haujaweka wazi orodha ya kikosi kilichosafiri kwa ajili ya mchezo dhidi yao na Prisons utakaoanza saa 10 leo.
Timu zote mbili zimejivuna kupigania alama tatu kuelekea mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka jijini Mbeya.
Yanga itashinda kwasababu mganga wao amewahalikishia kwa matokeo hauo
ReplyDeleteTaarifa iliyopo ni kocha kuomba wachezaji muhimu kubaki Dar kwa ajili ya mechi na Ryon Sport kutoka Rwanda...wachezaji tangu watoke Algeria wahajapata hata muda wa kufanya mazoezi wala kupumzika. Kocha akaona timu ya pili na wachezaji baadhi wabebe mzigo wa Kwenda Mbeya na wengine 16 wabaki Dar kwa ajili ya maandalizi
ReplyDelete