May 2, 2018




Wakati kikosi cha Yanga kikitarajia kuanza safari yake kuelekea nchini Algeria kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger, kumekuwa na sintofahamu juu ya safari hiyo.

Licha ya sintofahamu iliyojitokeza, salehjembe.blogspot.com imefanya jitahada za hali na mali kutaka kujua namna Yanga walivyojiandaa kuanza safari hiyo lakini viongozi wamekuwa hawapokei simu.

Yanga itakuwa na kibarua dhidi ya wapinzani hao wa Algeria, USM Alger katika mchezo wa mkondo wa kwanza utakaopigwa Mei 6 2018 nchini humo.

Haijajulikana sababu za viongozi hao kutopokea simu kwa takribani lakini taarifa za chini ya kapeti zinaeleza kuwa baadhi ya wachezaji wameweka mgomo kutokana na kutolipwa stahiki zao ikiwemo mishahara.

Hata hivyo uongozi licha ya kushindwa kupokea simu, leo umetangaza kuitisha kikao na Waandishi wa Habari kitakachofanyika majira ya saa 6 mchana kwenye makao makuu ya klabu.




6 COMMENTS:

  1. Swaumu inaendelea, duh. Poleni watani.

    ReplyDelete
  2. Wakimataifa msituangushe mbona mapema mnanza kutukatisha tamaa

    ReplyDelete
  3. Suala la kupokea simu ni lingine na suala la kusafiri ni la upande mwingine. Safari haiwezi kukosekana. Tusubili

    ReplyDelete
  4. Isije kutokea kama ya MTIBWA SUGER Maana inaonekana mtani jembe ameishiwa hadi nauli. Kama vp aende harafu akirudi aje msimbazi tumpe msaada

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic