UONGOZI YANGA WATOA KAULI KUHUSIANA NA WACHEZAJI AMBAO HAWAKUSAFIRI NA TIMU KAMA WATAKIPIGA NA PRISONS
Uongozi wa klabu ya Yanga umesema kuwa haujajua maamuzi ya kocha wake kuhusiana na wachezaji walioshindwa kusafiri na timu kuelekea Algeria kama wataungana na kikosi kitakachoelekea Mbeya kwa ajili ya mchezo wa ligi.
Ofisa wa Habari wa Yanga, Dismas Ten, amesema kuwa jukumu hilo litakuwa kwa Kocha wake, Mkongomani, Mwinyi Zahera, kama ataamua kuwaunganisha kwa ajili ya mchezo huo au asifanye hivyo.
Ten amesema hayo baada ya kikosi cha Yanga kuwasili jana kikitokea Algeria kushiriki mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger na kuambulia kichapo cha mabao 4-0.
Baadhi ya wachezaji ambao hawakusafiri ni Kelvin Yondani, Ibrahim Ajibu na Papy Kabamba Tshishimbi.
Ratiba ya Ligi Kuu Bara inaonesha kuwa Yanga watakuwa na kibarua dhidi ya Tanzania Prisons, Mei 10 2018 jijini Mbeya.
0 COMMENTS:
Post a Comment