KAULI TATA YA MKONGOMANI WA YANGA KUHUSU KIKOSI CHAKE KUPOTEZA DHIDI YA WAARABU
Kocha Mkuu wa Yanga, Mkongomani Mwinyi Zahera, amesema kikosi chake kilikwenda Algeria kikiwa na hofu ya kupambana na USM Alger katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika.
Zahera ameeleza kuwa Yanga ilikwenda na 'WATOTO' kauli ambayo inamaanisha wachezaji ambao hawakuwa na uzoefu katika mashindano ya kimataifa, jambo ambalo lilipelekea kufungwa mabao 4-0.
Kocha huyo ameeleza kuwa wachezaji wengi waliosafiri na timu kukipiga na Waarabu katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi hawakuwa wanajiamini kitu ambacho kilisababisha kupoteza mechi.
Zahera amezungumza hayo baada ya Yanga kuwasili nchini jana wakati akihojiwa na Waandishi wa Habari waliokusanyika Uwanja wa Ndege kuisubiri.
Yanga iliwakosa nyota wake kadhaa ikiwemo Kelvin Yondani, Obrey Chirwa na Papy Kabamba Tshishimbi ambao taarifa kutoka kwa uongozi wa Yanga walieleza kuwa wana matatizo binafsi yaliyopelekea kushindwa kusafiri.
0 COMMENTS:
Post a Comment