May 14, 2018



Kikosi cha Kagera Sugar kitakuwa mgeni wa mchezo wa ligi dhidi ya Simba Mei 20 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kagera inajiandaa kucheza na Simba baada ya kufanikiwa kuibuka na ushindi mnono katika mechi ya mwisho dhidi ya Njombe Mji kwa kuifunga mabao 3-1.

Ushindi huo umekuwa ni salaam ya kuja kutibua rekodi ya Simba ambayo haijapoteza mechi hata moja kwenye ligi msimu huu.

Kwa mujibu wa Kocha Msaidizi wa Kagera Sugar, Ally Jangalu, amesema kuwa ushindi dhidi ya Njombe unawapa nguvu ya kuzidi kufanya vizuri katika michezo ijayo ikiwemo Simba.

Ikumbukwe katika mechi ya mzunguko wa kwanza iliyopigwa January 22 kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Kagera, Simba waliibuka na ushidi wa mabao 2-0.

Janagalu amesema hivi sasa wanajipanga kuja kulipiza kisasi ili kuwaharibia Simba ambao hawajapoteza mchezo hata mmoja mpaka sasa.

3 COMMENTS:

  1. Hata Singida walisema wamepanga kuwaharibia simba

    ReplyDelete
  2. Walianza Yanga kusema watafia uwanjani mechi na Simba, wakaja Singida wakasema watatibua sherehe za ubingwa wa Simba na nyie yale yale. Maana mara ya mwisho akapigwa shabiki hadi kupoteza fahamu sijui tarehe 20, May 2018 itatokea nini mechi ya Simba Vs Kagera Sugar?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic