May 30, 2018


Na George Mganga

Wakati Yanga ikianza maandalizi ya kujiandaa na safari ya kesho kuelekea Kenya kwa ajili ya michuano ya SportPesa Super Cup, taarifa zinaeleza kuwa beki wake, Kelvin Yondani, ametimkia kusikojulikana.

Yondani hajacheza mchezo wowote tangu agungiwe na Bodi ya Ligi ya TFF baada ya kumtemea mchezaji wa Simba, Asante Kwasi katika mchezo uliowakutanisha watani hao wa jadi, Simba na Yanga, Aprili 29 2018 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa amelitolea ufafanuzi kuhusiana na kutopatikana kwa Yondani akieleza kuwa amepatwa na matatizo ya kifamilia hivyo atarejea kikosini siku yoyote.

Akizungumza na Radio EFM, Mkwasa amesema suala la mchezaji kutokuwa hewani kupitia simu yake haina maana ya kwamba hawezi kuonekana na akieleza kuwa ni jambo la kawaida pekee.

Mbali na hilo, Mkwasa amesema Yondani bado ni mchezaji wa wao kwa kuwa bado ana mktaba na Yanga licha ya kuwepo kwa tetesi kuwa Simba wanamuwinda kwa ajili ya kumsajili.

Yondani alifunguliwa kifungo chake kalba ya mechi dhidi ya Azam kufuatia kitendo chake cha kumtemea mate Kwasi katika mchezo dhidi ya Simba ambao Yanga walikubali kichapo cha bao 1-0.

6 COMMENTS:

  1. WE GEORGE MGANGA UTAKUWA MKE WA YONDANI MAANA NAONA UNAZIJUA KWELI HABARI ZAKE, EMBU TUAMBIE NA JANA ALILALA WAPI??

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ndala Bhana! Wakielezwa Ukweli Hujifanya Unawauma Wakati Ukweli Ni Kwamba Mabange (Yondani) Kakimbia Njaa Ya Jangwani Coz anakosa Hata Hela Ya Ganja.

      Delete
  2. Kila anapopotea mchezaji wa yanga viongozi hutoa sababu ya matatizo ya familia hasa mwaka huu ambako wachezaji zaidi ya kumi utasikia wana matatizo ya familia. Mbona matatizo hayo hatuyasikii kwengineko isipokuwa yanga tu? Msema kweli ni mpenzi wa Mungu

    ReplyDelete
  3. iisimba naona kabisa msemo wa raisi unaweza kutimia kama inasajiri kwa mihemko na kukomowana sioni chamaana watakachofanya yondani anashindwa kuisaidi timu yake leo atawezaje kuisaidia simba.

    ReplyDelete
  4. Aliyekwambia YONDANI yupo SIMBA ni nani?acha ujinga ndugu hatusajili wavuta bangi sisi.

    ReplyDelete
  5. Kumuhusisha Yondani na kusajiliwa Simba kunapotosha ukweli. Simba haina ukosefu wa beki . Yondani katokea Simba. Hana nidhamu nzuri uwanjani imedhihirika alipomtemea mate kwa makusudi mchezaji wa Simba Asante Kwasi. Kitendo cha ovyo ovyo sana. Mchezaji aliyetoka Simba kwenda Yanga ambaye unaweza kumvumilia kurudi Simba ni AJIBU basi. Ametoka Simba bila kuikashifu. Huyu anaweza kurudi. Mchezaji kama Kessy hana nafasi ya kurudi kwa mabaya aliyowafanyia Simba. Kessy mchezaji mzuri anajituma lakini aliiuza Simba uwanjani na kuwasaliti mchana kweupe.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic