Uongozi wa klabu ya Yanga umefunguka na kuwataka wapenzi wa soka nchini wafahamu kwamba lengo la wao kutaka kumchukua mshambuliaji wa Lipuli Adam Salamba ni kuiongezea nguvu safu ya ushambuliaji katika michezo ya kimataifa na wala siyo kumsajili kuitumikia Yanga kama wanavyodhani wao.
Ufafanuzi huo umetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Dismas Ten baada ya kutokea sintofahamu kwa mashabiki wa soka wakidhani kitengo wanachotaka kukifanya Yanga ni kutaka kumchukua mchezaji huyo moja kwa moja ili akawasaidie katika michuano ya ligi na vinginevyo.
“Watu wengi wanatafsiri hili jambo vibaya au tofauti, kanuni CAF zinaruhusu kusajili wachezaji watatu kwaajili ya mashindano ya Shirikisho Afrika na inaruhusu kumtumia mchezaji yeyote ambaye anachezea katika vilabu vya ndani ili mradi awe hajacheza mashindano ya kimataifa kwa hiyo ‘techinical bench’ walimuona Adam Salamba kuwa mchezaji mzuri na anaweza kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji katika kikosi chetu”, amesema Dismas.
Dismas ameendelea kwa kusema “ndio maana tukafanya jitihada za kuwaandikia barua Lipuli FC kwamba tunamuomba huyu mchezaji kwaajili ya kutusaidia na kutuongezea nguvu kwenye mechi za kimataifa na siyo kumsajili kama baadhi ya watu wanavyosema wao. Masuala ya usajili ni jambo jingine kama itatokea hivyo basi tutakwenda kwa Lipuli kuzungumza masuala hayo na kwenda hatua nyingine”.
Kwa upande mwingine, Dismas amewataka wanalipuli wasiwe na shaka na mchezaji wao Salamba kwa kuwa dirisha la usajili bado halijafunguliwa ila wanachokifanya wao nikutaka kuongeza nguvu katika kikosi chao ili waweze kupambana vilivyo katika mechi zao za kimataifa zinazoendelea kwa mujibu wa ratiba ya CAF.
CHANZO: SPOTI XTRA
Wakikubali kukuazimeni mpeni huyo mahela na muahidini mamilioni ya kumsajili. Bila ya shaka atakataa kurudi Lipuli na atakuwa wenu
ReplyDelete