May 8, 2018




Baada ya wachezaji baadhi wa Yanga kutoonekana dimbani kwa muda mrefu, uongozi wa Yanga umesema unahofia kuvunja nao mikataba kwa hofu ya kupata hasara.

Donald Ngoma na Amis Tambwe ni miongoni mwa wachezaji walioshindwa kuichezea timu hiyo kwa muda mrefu kutokana na kukumbwa na majeraha.

Kutokuwepo kwa wachezaji hao kumechangia kikosi hicho kushindwa kupata huduma yao ambao walikuwa mhimili mkubwa ndani ya timu.

Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa, amesema kuwa wana hofu ya kuvunja nao mikataba kwasababu itawalazimu kuwalipa fedha za uvunjaji.

Kauli ya Mkwasa imekuja kutokana na klabu hiyo kutokuwa vizuri kiuchumi kwa sasa tangu Mwenyekiti wao Yusuph Manji kutangaza kujiuzulu nafasi yake.

3 COMMENTS:

  1. Ndugu Saleh Jembe, naomba unifikishie ujumbe huu kwa uongozi wa Yanga. Kwanza ni aibu na ni hali inayokatisha tamaa ikionyesha wazo uwezo wa kufikiri na ubunifu wa viongozi wa Yanga umefika kikomo, haiwezekani mmezungukwa na lundo la mashabiki na wanachama bado mnalia njaa, yaani hata mwanamziki Diamond anawazidi viongozi wa Yanga katika ubunifu, Diamond ana mashabiki na anapata pesa kupitia mashabiki wake na makampuni yana mdhamini kwakuwa yanajua ana mashabiki wengi na leo amethubutu hata kuanzisha tv yake, iweje uongozi wa Yanga mnashindwa kuwa wabunifu? mnashauriwa hamshauriki au mmelogwa? Hata msanii mwanadada Shilole anapata pesa kutokana na mashabiki wake na biashara zake zinauzika kutokana na umaarufu wake. Uongozi uliopo Yanga upo kwenye usingizi wa pono, haujitambui haujielewi hoi bin taabuni, bado mna ndoto mheshimiwa Manji atarudi hizo ni ndoto za mchana. Yanga inaweza kuanzisha kampuni ya bahati nasibu ambayo wanachama na mashabiki wake wanaweza kununua hisa katika kampuni hii kama ilivyo katika kampuni za biko, tatu mzuka, moja bet nk na lengo la kampuni hii liwe ni kuchezesha mchezo wa bahati nasibu ambapo kila mshiriki atachangia sh 1000 kwa tiketi moja na zawadi za ushindi kwa washindi wa 3 zitoke mwishoni mwa mwezi, endapo watu 1000000 watacheza kila siku zitabatikana bilioni 1 kwa siku. Na kama watu laki 5 watacheza kila siku zitapatikana milioni 500 kwa siku basi hata wakicheza watu laki 1 kwa siku zitapatikana milioni 100 kwa siku sasa milioni 100 kwa siku 30 ni bilioni 3 na zile bilioni 1 kwa siku ni bilioni 30 kwa mwezi. Hili ni wazo langu tu na linaweza kuboreshwa zaidi. Kwa imani yanga Yanga au Simba ni timu tajiri zinazohitaji watu wabunifu na wenye uthubutu, timu hizi haziwezi kuwa tegemezi kwa watu endapo rasilimali watu iliyopo katika timu hizi itatumika vizuri. Uongozi wa Yanga kipindi hiki ndicho kipindi cha sahihi cha kufanya mageuzi, kipindi unapokabiliwa na shida fulani ndio wakati sahihi wa kutafuta dawa au uvumbuzi na uvumbuzi huu lazima uwe wa kudumu.

    ReplyDelete
  2. Matatizo siku zote yanapelekea kutafuta ufumbuzi na ugunduzi wa nia mbadala. Hivi kweli unasimama mtu mzima unasema kiongozi wetu baada ya kujiuzulu hatuna fedha, kumbe timu ya Yanga ilikuwa ya mtu siyo ya wanachama? Mlisema mmeanzisha wanachama kuchangia, kuna Sports Pesa, VODACOM, AZAM nk hizo fedha zinakwenda wapi? Basi wapelekeni hao wachezaji wakatibiwe ili waje kuitumikia timu, inakuwaje mnatuahidi watacheza na Simba wakati ukifika sababu kibao, uongozi badilikeni jamani!!!!!!!

    ReplyDelete
  3. Yaani kwa yanga pindi mchezaji tegemeo aliyejitolea na kuipa timu ubingwa akianguka husahau yote na njia mkato ni kuvunja mkataba na kumpa kwaheri ya kuonana. Tazama Simba wachezaji wapya kabla ya kufaidika nao na wakapata majeraha, Simba haikuwatupa bali harakaharaka wakapelekwa India kwa matibabu. Henyi ndugu msibabake kwa ahadi feki mkajikuta mkajikuta kwenye msala upitao na majuto ni mjukuu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic