May 8, 2018



Uongozi wa klabu ya Yanga umeilalamikia ratiba ya Ligi Kuu Bara msimu huu kwa kueleza kuwa inawabana kutokana na namna ilivyo.

Kupitia Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa, amesema kuwa ratiba hiyo si rafiki kulingana na namna ilivyopangwa haswa kuelelea mechi za mwisho kumaliza ligi.

Baada ya kutoka kushiriki mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger ya Algeria, Yanga walianza safari jana kurejea nchini na wanatarajiwa kuwasili mchana wa leo.

Ratiba inaonesha kuwa baada ya Yanga kuwasili, kesho mapema itawabidi wasafiri kuelekea Mbeya kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons, utakaopigwa Alhamis ya wiki hii.

Licha ya ratiba hiyo kupangwa na kupanguliwa kwa mara kadhaa, bado inaonesha kuibana Yanga ambayo inashiriki zaidi katika mashindano tofauti ukiachana na ligi kuu.


3 COMMENTS:

  1. Mkwasa ni mtu anaehishimika na watanzania wengi hasa wapenda soka si wasimba si wa Yanga wanamuheshimu Mkwasa lakini madai yake na malalamiko anayoyatoa kuhusu ratiba ya ligi kutokuwa rafiki na yanga ni ya kipuuzi. Mimi sijawahi kuona au kusikia duniani kwenye ligi moja kuna timu imeshacheza michezo minne zaidi alafu wenye faida ya viporo wakaanza kulalamikia ratiba. Mimi binafsi niliwaona Simba waungwana na mashujaa sana kukubali kuendelea kukamilisha ratiba ya mechi zao wakati wakijua yakwamba mpinzani wao wa karibu anafaida ya machi za viporo iwapo Simba angeteleza. Wakulalamika hapa ni Sumba wala sio yanga.
    kushiriki mashindano ya kimataifa wala isiwe sababu ya Yanga kujipangia ratiba .
    Nashindwa kuelewa labda yanga wanataka SIMBA amalize mechi zake zote za ligi ndio waanze kujipangia za kwao.

    ReplyDelete
  2. tatizo ni kwamba simba anashinda

    ReplyDelete
    Replies
    1. Naunga mkono hoja... Tatizo Mnyama anashinda ndio maana Viporo vinaonekana kama Friend mechi

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic