May 16, 2018


Na George Mganga

Dakika 90 za mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Yanga dhidi ya Rayon Sports kutoka Rwanda zimemalizika katika Uwanja wa taifa, Dar es Salaam kwa matokeo ya suluhu ya 0-0.

Mchezo huo ulionekana kwa kila timu kucheza kwa uangalifu zaidi huku wote wakikosa nafasi kadhaa za kufunga ikiwemo Yanga kupitia Chirwa aliyegongesha mwamba mnamo kipindi cha pili.

Mchezo ambao ni wa pili kwa timu zote mbili katika hatua ya makundi ya michuano hiyo unaiweka Yanga katika mazingira magumu ambapo mpaka sasa inakuwa imeambulia pointi moja pekee.

Ikumbukwe katika mechi iliyopita Yanga ilikubali kupoteza kwa jumla ya mabao 4-0 dhidi ya dhidi ya USM Alger huko Algiers, Algeria.

Wakati huo Rayon Sports inakuwa imejikusanyia alama 2 kwenye kundi hilo 'D' baada ya sare ya 1-1 dhidi ya Gor Mahia FC ya Kenya kwenye mechi yake ya kwanza iliyopigwa Kigali, Rwanda.

2 COMMENTS:

  1. Ukoxef wa xtricker utaigharim yanga

    ReplyDelete
  2. Huwezi ukamtegemea mchezaji mmoja mbele atafute mipira, ashambuliane na mabeki na kupata akili ya kufunga, hilo halipo. Hakuna jinsi tafuteni mshambuliaji kama Okwi na Bocco.

    Protas-Iringa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic