May 17, 2018


Kufuatia suluhu dhidi ya Rayon Sports katika mchezo wa jana wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi katika hatua ya makundi, Yanga imefikisha dakika 720 bila kupata matokeo.

Dakika hizo ambazo ni sawasawa na mechi nane kwa Yanga zimeendeleza rekodi mbovu kwa Yanga kushindwa kupata alama tatu kwenye mechi hizo.

Tangu Kocha George Lwandamina aondoke kikosi cha Yanga kimeshindwa kupata pointi tatu kuanzia kwenye mechi za Kombe la Shirikisho Afrika mpaka Ligi Kuu Bara.

Ni rekodi ya aina yake ambapo kikosi hicho sasa kipo chini ya Kocha Msaidizi Shadrack Nsajigwa pamoja na Noel Mwadila huku Kocha Mkuu mtarajiwa, Mwinyi Zahera, akiwa bado hajaanza kukiongoza kwenye ligi.

Mbali na kufikisha dakika 720, Yanga imekuwa ikiandamwa na wachezaj wengi ambao wamekuwa majeruhi ikiwemo Donald Ngoma ambaye amekosekana Uwanjani kwa muda mrefu.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic