BAADA YA KUPOTEZA FAINALI, SINGIDA YAKUBALI MATOKEO , YATOA PONGEZI KWA MTIBWA
Baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-2 dhidi ya Mtibwa Sugar FC, uongozi wa Singida United umekubali matokeo huku ukisema utajipanga wakati ujao.
Mkurugenzi wa timu hiyo, Festo Sanga, amesema kuwa Mtibwa walisakata kambumbu la maana leo hivyo walistahili kupata matokeo.
Sanga amewapongeza Mtibwa kwa ushindi huo uliowawezesha kubeba taji hilo na kufungua milango ya kuiwakilisha Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
"Tumekubali matokeo ya leo na huu ndiyo mpira, kiufupi tunawapongeza Mtibwa Sugar kwa mchezo mzuri waliouonesha Uwanjani na kufanikiwa kuibuka washindi, nawatakia kila kheri katika mashindano ya kimataifa" amesema Sanga.
Mtibwa Sugar wamechukua taji hilo kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwake huku fainali hiyo ikifanyika kwa mara ya kwanza pia jijini Arusha na kuhudhuriwa na maelfu ya watazamanji Uwanjani.
0 COMMENTS:
Post a Comment