June 2, 2018

TRY AGAIN


Uongozi wa klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam, umesema kamwe hakuna mchezaji ambaye inamhitaji ataondoa.

Simba imesema inaamini hakuna nafasi kwa wao kumuachia mchezaji ambaye inamuhitaji.

Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdallah 'Try Again' amesema hawatamuachia yoyote aondoke, hasa wanayemhitaji.

“Kama mchezaji tunamhitaji, nakuhakikishia hawezi kuondoka. Wale ambao mikataba yao imeisha tunaendelea nao na mazungumzo na kama tunawahitaji, basi nikuhakikishie hawawezi kuondoka,” alisema.

Baadhi ya wachezaji wa Simba wamekuwa katika mazungumzo na uongozi wa klabu hiyo ukiwataka kuongeza mkataba baada ya kumaliza msimu mzima wakiwa wamepoteza mechi moja tu.

1 COMMENTS:

  1. Sawa sasa nateremsha pumzi. Yanga nao wakimnyatia. HAHAHAA

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic