June 18, 2018




Ndege aina ya Air Bus A319-100 iliyokuwa imewabeba wachezaji wa Saudi Arabia imeshika moto nchini Urusi.
Ndege hiyo ilikuwa imewabeba wachezaji wa Saudi Arabia ikisafiri kwenda katika mji wa Rostov kwa ajili ya mechi yao ya pili dhidi ya Uruguay,

Katika mechi ya kwanza Saudi Arabia walifungwa mabao 5-0 na wenyeji Urusi na hadi sasa ndiyo timu iliyofungwa mabao mengi zaidi.


Hata hivyo, ndege hiyo ilikuwa imekaribia kutua katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Don, bawa moja la kulia lilishika moto na kusababisha hofu.

Baadaye ilifanikiwa kutua salama huku magari ya kuzima moto yakiwa yameizunguka na kufanikiwa kuuzima moto huo huku wachezaji na viongozi wa Saudi Arabia wakifanikiwa kushuka salama salimini.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic