June 18, 2018


Ubelgiji imeshinda kwa mabao 3-0 huku mshambuliaji wa Manchester United Romelu Lukaku akipiga bao mbili.

Ubelgiji imeitwanga Panama kwa mabao hayo 3-0 katika mechi yao ya kwanza ya Kombe la Dunia hatua ya makundi na sasa Wabelhiji wanaongoza kundi G lenye timu za England na Tunisia pia zitakazocheza hivi punde.

Lukaku alifunga bao la pili kwa kichwa cha kuchupa akipokea pasi ya Kevin De Bruyne kabla ya kuongeza la tatu katika dakika ya 75 kwa pasi nzuri ya nahodha wake, Eden Hazard.
Kabla Mertens alifunga bao safi katika dakika ya 47, akipiga shuti safi la kutoka pembeni mwaka uwanja na kuifanya Ubelgiji kuongoza mwanzoni mwa kipindi cha pili.











0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic