DIAMOND AALIKA NDUGU JAMAA NA MARAFIKI KUSHEREHEKEA EID NYUMBANI KWAO TANDALE
Na George Mganga
Wakati Waislam leo kote duniani wakisherehekea sikukuu ya kumalizika kwa Mwezi Mtukufufu wa Ramadhan (Eid), Msanii wa muziki wa kiazi kipya, Diamond Platnumz, ameamua kufuturisha ndugu, jamaa na marafiki nyumbani kwao.
Platnumz ambaye ni moja ya wasanii wakubwa Tanzania na Afrika Mashariki, amemua kufanya tukio hilo ili kuwakutanisha watu mbalimbali ili kusherekea kwa pamoja katika sikukuu hii ya Eid.
Kupitia Ukurasa wake wa Instagram, Platnumz ameandika kuwakaribisha ndugu jamaa na marafiki nyumbani kwao alipokulia, Tandale kwa ajili ya kutoa mkono wa Eid Mubarak.
"Leo kuanzia saa TANO ASUBUHI nitakuwepo nyumbani TANDALE nikitoa mkono wa EID MUBARAK kwa ndugu jamaa na marafiki. Tafadhali nawakaribisha wote" aliandika.
0 COMMENTS:
Post a Comment