June 15, 2018


Na George Mganga

Beki wa klabu ya Yanga, Kelvin Yondani, yuko nyumbani kwao Mwanza hivi sasa kufuatia mapumziko ambayo wachezaji wote wa klabu hiyo kupewa na uongozi.

Yondani amemua kujumuika na mke wake kuelekea nyumbani kwao na mapema Juni 25 atarejea tena kambini kuanza kujiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Mbali na Yondani, wachezaji wengine wa kimataifa nao wamerejea makwao kwa ajili ya likizo hiyo maalum ambapo nao watarudi kujiunga na kikosi tarehe tajwa hapo juu kuanza kuwawinda Gor Mahia FC ya Kenya.

Yanga itakuwa na kibarua ugenini dhidi ya Gor Mahia katika mchezo huo wa Kombe la Shirikisho ikiwa ni baada ya kulazimishwa kupoteza dhidi ya MC Alger kwa bao 4-0 na kwenda suluhu ya 0-0 na Rayon Sport ya Rwanda.

Kuelekea mchezo huo Yanga inapaswa kupata matokeo ili kujitengenezea nafasi nzuri ya kufuzu kwenda hatua inayofuata kutokana na kukosa alama tatu muhimu katika michezo iliyopita.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic