June 14, 2018


Baada ya kufanikiwa kutwaa tuzo ya Mo, kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba, Shiza Kichuya, amesema atazidi kupambana zaidi ili kubeba nyingine mwakani.

Kichuya alichaguliwa kuwa kiungo bora wa Simba kwa msimu wa 2017/8 baada ya kuonesha kiwango maridhawa na kufanikiwa kubeba tuzo hizo zinazojulikana kama Mo Simba Awards.

Kitendo cha kutwaa tuzo hiyo kimemfanya Kichuya atoe ahadi ya kujituma zaidi kwa mara nyingine katika msimu ujao ili aweze kuchukua nyingine.

Mchezaji huyo tegemeo wa Simba alijiunga na kikosi hicho msimu wa 2016/17 akitokea Mtibwa Sugar sambamba na wachezaji wenzake, Mohammed Ibrahim, Ally Shomari na Mzamiru Yassin.

Mchezaji huyo alijizolea umaarufu mkubwa Simba baada ya kumfunga Ally Mustapha 'Barthez' kwa mpira wa kona ya moja kwa moja katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga uliopigwa msimu wake wa kwanza akiwa na Simba.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic