June 12, 2018


Na George Mganga

Baada ya kumalizika kwa halfa ya ugawajwi wa tuzo za Mo jana kwenye Ukumbi wa Hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam, kikosi cha Simba kimepewa mapumziko ya wiki moja.

Simba wanenda mapumziko ikiwa ni siku kadhaa wametoka kushiriki mashindano ya SportPesa Super Cup mjini Nakuru ambapo walifanikiwa kufika hatua ya fainali na kupoteza kwa jumla ya mabao 2-0 dhidi ya Gor Mahia FC.

Mapumziko hayo mafupi yatafuatiwa na maandalizi ya michuano ya KAGAME CUP yanayotarajiwa kuanza Juni 28 jijini Dar es Salaam.

Katika mashindano hayo Simba ipo kundi C ikiwa imepangwa na klabu za Yanga ambayo imeomba kujitoa, Dakadaha ya Somalia na St. George ya Ethiopia.

Michuano hiyo inayotaaji kuanza Juni 28 2018 itamalizika Julai 23 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic