HOTUBA YA MOHAMMED DEWJI KWENYE TUZO ZA SIMBA
MHE MGENI RASMI, DKT. HAMISI KIGWANGALLA, WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII,
MHE MGENI MAALUMU, MZEE WETU ALI HASSAN MWINYI, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,
KAIMU RAIS WA SIMBA,
WAHESHIMIWA VIONGOZI WA SERIKALI,
WAHESHIMIWA WABUNGE,
WAHESHIMIWA MABALOZI,
WAJUMBE WA KAMATI WA UTENDAJI YA KLABU YA SIMBA,
VIONGOZI WA TFF,
VIONGOZI WA BODI YA LIGI,
VIONGOZI WA BARAZA LA MICHEZO LA TAIFA,
WADHAMAINI WA KLABU YA SIMBA,
MWENYEKITI NA WAJUMBE WA KAMATI YA ZABUNI YA KLABU YA SIMBA,
WAJUMBE WA KAMATI YA UWEKEZAJI YA KLABU YA SIMBA,
WANACHAMA WENZANGU,
MARAFIKI ZANGU,
WANAHABARI,
WAGENI WAALIKWA MABIBI NA MABWANA
ASALAAM ALAYKUM.
SIMBA… (NGUVU MOJA)
SIMBA… (NGUVU MOJA)
THIS IS… (SIMBA)
AWALI YA YOTE TUMSHUKURU SANA MWENYEZI MUNGU KWA KUTUWEZESHA KUFIKIA SIKU HII YA LEO. NI SIKU KUBWA SANA KWETU KWENYE SHEREHE HII YA TUZO KWA WATU WALIOI-WEZESHA KLABU YETU YA SIMBA KUFIKA HAPA ILIPO SASA.
KIPEKEE, TUMSHUKURU TENA MWENYEZI MUNGU AMBAYE AMETUWEZESHA KWA MATAKWA YAKE KWA MARA YA KWANZA KUKUTANA BAADA YA KUSHINDA ZABUNI KATIKA KLABU YETU YA SIMBA. NA KUANDAA TUZO AMBAZO ZITAKA-ZOTOLEWAKWA WACHEZAJI, BENCHI LA UFUNDI, VIONGOZI, MASHABIKI NA WAPENZI MBALIMBALIWA SIMBA.
NICHUKUE NAFASI HII KUISHUKURU SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA INAYOONGWA NA MHE. RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI KWA JITIHADA ZA KUSAIDIA NA KUKUZA UCHUMI WETU, AMBAO KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE, UMETOA FURSA KWETU SISI KUWEZA KUWEKEZA KATIKA MAENEO MBALIMBALI IKIWEPO KATIKA KLABU HII. LAKINI PIA KUWASHUKURU WASAIDIZI WAKE KUANZIA MAKAMU WA RAIS, WAZIRI MKUU NA MAWAZIRI WOTE KWA KAZI KUBWA WANAYOI-FANYA YA KULIJENGA TAIFA HILI.
MHE. MGENI RASMI NA WAGENI WAALIKWA, KAMA MNAVYOFAHAMU KWAMBA KLABU YETU YA SIMBA IMEINGIA KATIKA MFUMO MPYA WA UENDESHAJI AMBAO UMETUPA NAFASI YA KUWEKEZA KATIKA KLABU HII TUNAYOISHABIKIA SANA.
MARA KADHAA NA HASA KATIKA KIPINDI HIKI CHA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI, NIMEKUWA NIKITUMIA SEHEMU YA MUDA WANGU KUJIULIZA? KWANINI MUNGU AMENIFANYA NIWE NA MAPENZI MAKUBWA KIASI HIKI NA KLABU HII.?LAKINI NAAMINI HILI NI JUKUMU AMBALO NIMEPEWA NA MWENYEZI MUNGU ILI NIIFANYIE MAZURI KLABU HII.
KLABU YETU INA HISTORIA KUBWA KATIKA SOKA LA HAPA NCHINI, AFRIKA MASHARIKI, NA AFRIKA KWA UJUMLA, LAKINI HATUKUWA NA UTARATIBU WA KUTOA TUZO KWA WENZETU AMBAO WALIJITOA KWA MOYO WAO WOTE, ILI KUHAKIKISHA TUNAPATA MAFANIKIO KATIKA MICHUANO MBALIMBALI AMBAYO TUNASHIRIKI.
KUNA MASHABIKI WAMEPOTEZA MAISHA YAO KWA AJILI YA SIMBA.KUNA MASHABIKI WANATUMIA SEHEMU KUBWA YA MUDA WAO KWA AJILI YA SIMBA. KUNA VIONGOZI WANAFANYA KAZI KWA BIDII SANA ILI TU. SIMBA IFANIKIWE. KUNA WACHEZAJI WETU WANACHEZA KWA KUJITUMA SANA, ILI SIMBA IPATE MAFANIKIO.KUNA BENCHI LA UFUNDI AMBALO LINAHAKIKISHA LINATUMIA KILA MBINU ILI TU TUPATE MATOKEO MAZURI.
KWA MFANO, TULIKUWA NAYE MCHEZAJI WETU MAREHEMU HUSSEIN TINDWA, AMBAYE ALIFARIKI DUNIA NDANI YA UWANJA, HUKU AKIITUMIKIA KLABU YETUILIPOKUWAIKICHEZA NA MABINGWA WA ZAMANI WA NIGERIA, KLABU YA RACCAH ROVERS MWAKA 1979. HUYU TUNA KILA SABABU YA KUMKUMBUKA,YEYE NA WENGINE KAMA OTHMAN MAMBOSASA, OMARI MAHADHI BIN JABIL, PATRICK MAFISANGO, MOHAMED KAJOLE, ADAMU SABU, EDWARD CHUMILA, MARTIN KIKWA, NA WACHEZAJI WENGINE WENGI WALIOTANGULIA MBELE YA HAKI. MUNGU AWAREHEMU NA AZILAZE ROHO ZAO MAHALI PEMA PEPONI. AMEEN
KWA RUKHSA YAKO MHE. MGENI RASMI NAOMBA TUSIMAME KWA DAKIKA MOJA ILI TUWAENZINA KUWAKUMBUKA PAMOJA NA KUTOA HESHIMA KWA MALEGENDARIES WETU HAWA.
PAMOJA NA NYOTA WETU HAWA WALIOTANGULIA MBELE YA HAKI, KLABU YA SIMBA IMETOA NYOTA WENGI SANA KUANZIA KARNE ILIYOPITA MIAKA YA 60 MPAKA HIVI LEO. MIONGONI MWAO NI MBARAKA MOHAMED, ABDALLAH KIBADEN, MTEMI RAMADHANI, ZAMOYONI MOGELA, MALOTA SOMA (BALL JUGGLER), SELEMANI MATOLA NA WENGINE AMBAO HAKUNA ASIYEJUA WALICHOI-FANYIA SIMBA NA TAIFA HILI KWA UJUMLA.
ILINICHUKUA MUDA KUFIKIRIA NI JAMBO GANI TUNAWEZA KUWAFANYIA WENZETU WALIO-ITENDEAMAMBO MAKUBWA KLABU. NA PIA KUWAINSPIRE WACHEZAJI WETU WA SASA, ILI WAWEZE KUJUA THAMANI YA KUCHEZEA SIMBA NA UKUBWA WA KLABU HII. HAPO NDIPO WAZO LA KUTOA TUZO ZA MO SIMBA LILINIJIA. NINAAMINI KWAMBA HII ITAKUWA NI NJIA BORA SANA YA KUTAMBUA MCHANGO WAO AMBAO UMEIWEZESHA SIMBA KUFIKA HAPA BAADA YA MIAKA 81 TANGU KUANZISHWA KWAKE.
HAIKUWA KAZI RAHISI, KWANI BAADA YA KUPATA WAZO LA TUZO NILIKUWA NA KAZI NYINGINE YA KUHAKIKISHA KUNAKUWA NA VIPENGELE AMBAVYO VITAGUSA KILA SEHEMU KWA WATU AMBAO JUHUDI ZAO ZIMESAIDIA SIMBA KUFIKAHAPA, KUANZIA KWA WACHEZAJI, BENCHI LA UFUNDI, VIONGOZI, MASHABIKI NA MATAWI YA SIMBA.
ILIKUWA KAZI KWELIKWELI, NA BAADAE NILIPATA VIPENGELE 16 AMBAVYO KWA HAKIKA VITAMGUSA KILA MMOJA WETU KUTOKANA NA JUHUDI ZAKE KWENYE KLABU HII.
ILI KUPATA WASHINDI HALALI, TULIONA NI VYEMA KAZI YA KUCHAGUA WASHINDI NIWAACHIE MASHABIKI WENZANGU AMBAO WALIPATA NAFASI YA KUPIGA KURA KUPITIA TOVUTI YA MOSIMBAAWARDS.CO.TZ NA KURASA ZA SIMBA ZA TWITTER, FACEBOOK NA INSTAGRAM.LAKINI PIA TULITEUA KAMATI AMBAYO ILIHUSISHA WADAU MBALIMBALI WA SOKA HAPA NCHINI KAMA TFF, BODI YA LIGI, MAKOCHA WA ZAMANI WA TIMU YA TAIFA, WACHEZAJI WA ZAMANI WA SIMBA, WADHAMINI NA WANAHABARI. NA KATIKA HILI NAPENDA KUCHUKUA NAFASI HIIKUISHUKURU KAMATI KWA KAZI KUBWA WALIYOIFANYA USIKU NA MCHANA ILI KUHAKIKISHA SHUGHULI HII INAFANIKIWA.
USHINDANI ULIKUWA NI MKUBWA SANA, HIVYO KILA KIPENGELE WALICHAGULIWA WATU WATATU, NA HII HAIMAANISHI KWAMBA AMBAO HAWAKUPATA NAFASI YA KUJUMUISHWA KATIKA VIPENGELE VYA TUZO ZA MWAKA HUU KUWA SIO BORA, BALI ILIKUWA NI LAZIMA KILA KIPENGELE WAPATIKANE WATU WATATU KWA AJILI YA KUPIGIWA KURA.
KWANI KAMA MNAVYOFAHAMU TIMU YETU INA WACHEZAJI WENGI WENYE VIWANGO AMBAVYO HAVIPISHANI SANA. HIVYO USHINDANI ULIKUWA NI MKUBWA, LAKINI MWISHO WA SIKU LAZIMA MSHINDI APATIKANE. BAADHI YA VIPENGELE AMBAVYO VILIKUWA NA USHINDANI MKUBWA NI KIPENGELE CHA MCHEZAJI BORA NA GOLI BORA, KWANI TULITOA NAFASI KWA MASHABIKI WENYEWE NDIO WACHAGUE.
NAOMBA NITUMIE NAFASI HII KUWAOMBA WACHEZAJI, BENCHI LA UFUNDI, VIONGOZI NA MASHABIKI, AMBAO WATASHINDA TUZO TUNATEGEMEA KUONA MKIZIDI KUONGEZA JUHUDI ZAIDI ILI KLABU YETU IZIDI KUSONGA MBELE KWA KUPATA MAFANIKIO. NA KWA AMBAO WATAKOSA NIWATIE MOYO KWAMBA HUU SIO MWISHO WA TUZO HIZI. ZITAKUWEPO KILA MWAKA INSHALLAH, HIVYO MKIJITUMA ZAIDI LABDA MWAKANI MNAWEZA KUWA MOJA YA WASHINDI WA TUZO KATIKA VIPENGELE MBALIMBALI AMBAVYO TUTAVIWEKA.
MWISHO, NAPENDA KUWASHUKURU WATU WOTE TULIOWAALIKA KWA KUKUBALI KUITIKIA MWITO WETU. MWENYEZI MUNGU AWAJALIE. MUNGU IBARIKI SIMBA. MUNGU IBARIKI TANZANIA. MUNGU IBARIKI AFRIKA.
AHSANTENI SANA KWA KUNISIKILIZA…
THIS IS… (SIMBA
0 COMMENTS:
Post a Comment