June 17, 2018


Tatizo siyo fedha, kwani Mohammed Dewji ‘Mo’ anaweza kuzitoa isipokuwa masharti magumu aliyoipa Simba ndiyo sababu ya kiungo mkabaji wa timu hiyo, Said Ndemla asuesue kusaini mkataba mpya wa kuendela kubaki kikosini humo.

Simba na kiungo huyo hivi karibuni wameshindwa kufikia makubaliano ya kusaini mkataba wa miaka miwili utakaomuwezesha kuendelea kuichezea Simba.

Awali, ilielezwa kuwa dau kubwa la usajili ambalo linalofikia shilingi milioni 70 alilolitaja ili aongeze mkataba wa kuichezea Simba kwenye msimu ujao wa Ligi Kuu Bara lilikuwa tatizo.

Kwa mujibu wa chanzo kuwa, meneja wa mchezaji ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kipindi cha utawala wa Jakaya Kikwete ndiye anayesimamia mkataba wake.

Mtoa taarifa huyo alisema, katika masharti hayo aliyoyatoa ni lazima yawepo kwenye mkataba ni lazima kiwepo kipengele cha yeye kucheza mechi na siyo kukaa benchi kama ilivyokuwa kwenye misimu miwili iliyopita ya ligi.

Aliongeza kuwa, katika suala la fedha ya usajili tayari wamelimaliza na kufikia muafaka mzuri na kikubwa wanachovutana katika kipengele hicho cha yeye kucheza katika kila mechi bila ya kujali nafasi atakayopangwa.

“Kikubwa anataka kuwepo kwenye timu kwa faida kwa maana ya kupata nafasi ya kucheza kama ulivyoona misimu miwili iliyopita, Ndema aliishia kusotea benchi wakati bado ana uwezo mkubwa wa kucheza, hivyo hataki kitu hicho kijitokeze tena akiwa na Simba,” alisema mtoa taarifa huyo.

Simba hivi karibuni kupitia kwa Kaimu Rais wa timu hiyo, Salim Abdallah alisema kuwa: “Timu yetu haitamruhusu mchezaji yeyote wanayemuhitaji kuondoka Simba kwa wale waliomaliza mikataba akiwemo Ndemla.”

Ndema ni mchezaji huru hivi sasa kwa mujibu wa kanuni anaruhusiwa kufanya mazungumzo na klabu nyingine na kusaini mkataba wa kuichezea. Yanga inatajwa kumuwinda mchezaji huyo ingawa duru za ndani ya Simba zinasema kwamba uwezekano way eye kwenda Jangwani ni mdogo.


CHANZO: CHAMPIONI

15 COMMENTS:

  1. Masharti hayo ni magumu sana kwa nafasi anayocheza ni mtihani kwa waalimu

    ReplyDelete
  2. Hilo linatakiwa kuwa sharti au kiwango?

    ReplyDelete
    Replies
    1. umeona eeehh, hawa wachezaji wetu wanataka wacheze wakati kwenye mazoezi hawamshawishi kocha. Kocha ndiye anayeamua mchezaji achezi kulingana na performance yake kwenye mazoezi

      Delete
  3. Kiwango ndokitaamua dogo acha utoto unatakiwabkukua na kuonyesha thamani yako iliende mbele zaidi

    ReplyDelete
  4. Ndemla ni mwanaume wa dhati tatizo ni simba kuleta walimu waliokariri taaluma ya mpira

    ReplyDelete
  5. Zile hadithi za kwenda Sweden zimeisha? Magazeti ya kibongo kwa uongo! Endelezeni ile hadithi

    ReplyDelete
  6. haiwezekani kumpangia kocha. Sharti lisilowezekana. Jitihada binafsi ndio zinamfanya coach aridhike na kumpanga. Shida wachezaji wa kibongo haswa wanaochipukia hawajitambui. kipaji pekee hakitoshi, Kuridhika na kipaji hakuna hatua yoyote atakayopiga.Mafanikio ni juhudi binafsi ktk mazoezi

    ReplyDelete
    Replies
    1. kaka unajua mpira, hongera kwa mawazo yako

      Delete
  7. Huwezi kumpa Kocha sharti la kukupanga ucheze mechi hata kama unaboronga upangwe tu?? haiwezekani, aende salama.

    ReplyDelete
  8. Aondoke tuu Simba haipangiwi masharti ya kulazimisha kuchezeshwa. Huyo Okwi na Bocco hawajaweka sharti hilo kuliko dogo?

    ReplyDelete
  9. Tuwe wawazi, viwango vya wachezaji, Simba waliomaliza msimu, wale walikokuwa wanapangwa viwango vyao vilikuwa sawa na cha Ndemla.
    Alipaswa apewe nafasi pia.

    ReplyDelete
    Replies
    1. kocha ndiye mwenye jukumu la kumpanga mchezaji uwanjani kulingana na uwezo anaouonesha katika mazoezi na mechi anazopangwa. Mchezaji anapaswa aoneshe ubora wake, amshawishi kocha sio kujaa sifa

      Delete
  10. hayo ni miongoni mwa masharti batilifu tangu mwanzo, ikumbukwe mkataba ni maagano ya pande mbili naona hapo anavutia kwa upande mmoja.. ................kuna masharti ambayo hata iweje lazima kuwe na sura ya kibinadamu mathalani amefiwa na mtu muhimu anaumwa itabidi masharti ya mkataba yafuatwe hata ikilazimu kumleta kwa ambulance uwanjani madhali mkataba unasema acheze kila mechi? ......la hasha.......Ndemla ni mchezaji anayeheshimika sana Simba na amekuwa mtulivu kwa muda mwingi nakumbuka jhata alipewa tuzo na mmoja wa wadau, tunaenzi mchango wake na pia tusigepeneda kioaji chake kipotee kwa kukaa benchi, ni vyema kuwekana wazi tu kama bado anaipenda simba na simba bado inampenda .......asaini mktaba mpya kwa kiango stahiki na afanye jitihada za kukuza kiwango chake apate namba ya kudumu kikosini ..............

    ReplyDelete
  11. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  12. Kocha ndiye anayeamua mchezaji achezi kulingana na performance yake kwenye mazoezi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic