June 17, 2018


Timu ya Nigeria kutoka Afrika imeungana na Morocco pampja na Misri kupoteza michezo yao ya awali dhidi ya Croatia kufuatia kichapo cha mabao 2-0.

Kipigo hicho kutoka Croatia kinatengeneza rekodi na taswira mbaya kwa timu za Afrika kutokana na kushindwa kupata matokeo hata sare.

Mabao ya Croatia yamefungwa na Etebo aliyejifunga katika dakika ya 32 kipindi cha kwanza na la pili likitiwa kimiani na Luca Modric kwa njia ya tuta katika dakika ya 71.

Matokeo ya mchezo huo yanawafanya Argentina wawe nafasi ya mwisho kwenye kundi D huku Croatia ikishika namba 1 kwa kunyakua alama zote tatu.

Argentina na Iceland zote zipo sawa kufuatia sare yao yao baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya mabao 1-1.

1 COMMENTS:

  1. heading umekosea,,,, sio ya nne bali ya tatu coz tunisia na senegal bado hawajacheza

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic