June 8, 2018



Baada ya kushuhudia mechi ya jana dhidi ya Kakamega HomeBoyz FC, inaelezwa kuwa Kocha Mkuu wa Simba, Pierre Lechantre na wa viungo, Aimen Habib, leo asubuhi wamekwea pipa kutoka Kenya kurejea Tanzania.


Makocha hao wameondoka nchini humo ambapo Simba inashiriki michuano ya Kagame ili kuja kujua mustakabali wa mikataba yao kutoka kwa uongozi wa juu.

Inaelezwa kuwa Lechantre na Habib walisusa kukaa kwenye benchi la ufundi jana wakati Simba ikicheza mchezo wa nusu fainali ya mashindano ya Super Cup na badala yake Kocha Msaidizi, Masoud Djuma akachukua nafasi hiyo.

Taarifa zinasema makocha hao wamerejea Tanzania kujua kinagaubaga kama wataweza kuongezewa mkataba mwingine kama ambavyo imeelezwa kuwa wanahitaji mkataba mwingine.

Mbali na kurejea Tanzania, taarifa zilizo chini ya kapeti zinasema kuwa uongozi wa Simba hautawaongezea mkataba wake na badala yake timu itaendelea kuwa na Djuma kwa kipindi hiki.

Aidha kumekuwa kunaelezwa kuwa Kocha huyo kutokuwa na maelewano mazuri na msaidizi wake, jambo ambalo linatajwa kuwa sehemu mojawapo ya yeye kuhusishwa kuondoka klabuni hapo.

Lechantre amesepa zake Kenya wakati Simba ikiwa katika maandalizi ya kukipiga dhidi ya Gor Mahia FC kwenye mchezo wa fainali ya Super Cup Jumapili ijayo.

Kocha Lechantre alikuja Simba kuchukua mikoba ya Mcameroon, Joseph Omog, alisaini mkataba wa miezi 6 pekee unaomalizika siku chache zijazo.

3 COMMENTS:

  1. Naende zake kwani kaizorotesha Simba ambapo alikabidhiw ikiwa na kiwango cha juu kutoka kwa Muhandisi Masoud na si kaona yeye mwenyewe jinsi alivofedheheka na matokeo ambapo alifikiri kukosekana kwake mnyama angeligaragazwa

    ReplyDelete
  2. Ushauri wangu kwa Uongozi wa Klabu ya SIMBA: Kocha huyu na huyo wa viungo wote wawili WAONDOKE ZAO. Kwa kuamua kususa timu hiyo tu inatosha kuonyesha hawafai kabisa. Kukosa nidhamu ya hali ya juu. Isipokuwa, hapana kuvunja mkataba waacheni wakae tu Dar es Salaam wasubiri kwisha kwa mkataba wao waondoke zao.

    ReplyDelete
  3. Masoud Djuma ni kocha ila Watanzania bado kwa kiasi kikubwa tumetawaliwa na mawazo tumwa ya kuto heshimu na kuthamini uwezo wa mtu mweusi au muafrika. Nakumbuka wakati SIMBA inamkabidhi timu Masoud Djuma baada ya kuondoka Omog,wajuaji walichonga mno na wengine walifika mbali zaidi kwa kusema wao wanauwezo kuliko Mrundi.Lakini kusema na vitendo ni vitu viwili tofauti kabisa kwani walioanza kuthibitisha kuwa Masoud Djuma ni kocha mwenye uwezo ni wachezaji wenyewe. Wachezaji kama Nicolas Gayan au hata Shomari kapombe pengine kama si ujio wa Masoud Djuma tungelishawasahu. Vipi Said Ndemla? baada ya kuondoka Omog Masoud Djuma alimrejesha katika ubora wake yuko wapi sasa? Vipi Muzamiru Yasini? Kwa kipindi kifupi alichoisimamia Simba Masoud Djuma ameonyesha uwezo wa hali ya juu si wa kuiongoza timu kupata ushindi tu bali hata kuwasidia wachezaji mmoja mmoja kuinua viwango vyao lakini baadhi ya watu hawakuacha kumsakama,ooh analipwa mashahara mkubwa,ooh analala hoteli ya bei mbaya so what? sasa kama wewe ni kocha wa kitanzania unajiamini kuwa una uwezo wa kuifundisha simba au yanga kwanini ulilie kuwa kocha Simba au Yanga peke yake? Katika kazi ambayo mahitaji yake ni makubwa kama unaimudu vizuri basi ukocha ajira zimejaa ukienda hata hapo kenya wanatafuta makocha wenye uwezo na si lazima kufanya kazi Tanzania tu. Mimi na namfananisha Masoud Djuma na Curkovici kocha aliewahi kuifundisha simba hapo nyuma ni miongoni mwa makocha ambao Simba walipaswa kudumu nae lakini ndio hivyo tena. Simba wanapaswa kumuamini Masoud Djuma na kumtafutia msaidizi asiekuja kumletea majungu katika kazi maana sisi Watanzania ndio hivyo tena.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic