June 4, 2018


Kocha Msaidizi wa Yanga, Noel Mwandila, ameweka bayana sababu zilizoleteleza kutolewa katika mashindano ya SportPesa Super CUP nchini Kenya na KK. HomeBoyz.

Yanga imeyaaga rasmi mashindano hayo kwa kupigwa kichapo cha mabao 3-1 kwenye Uwanja wa Afraha uliopo Nakuru, Kenya.

Akizungumza mara baada ya mchezo kumalizika, Mwandila amesema sababu iliyopelekea Yanga kushindwa kupata matokeo ni majeruhi ambao wanaiandama timu yake.

Mbali na majeruhi, Mwandila ameeleza kuwa Yanga imewakosa wachezaji 7 ambao ni tegemeo ndani ya kikosi chake na wengine akisema wamebaki Tanzania.

Baada ya kuondolewa, Yanga sasa inatarajia kuanza safari ya kurejea Tanzania pamoja na JKU ya Zanzibar ambayo pia imeondolewa kwa kipigo cha mabao 3-0 na Gor Mahia FC.

Simba SC na Singida United ndizo klabu pekee zilizosalia kwenye mashindano hayo hivi sasa.

3 COMMENTS:

  1. Yanga haikosi sababu. Sema kweli kuwa wachezaji wana njaa hawajapata malipo yao tangu miezi kadha iliyopita na wana njaa na kupoteza morali na mwisho wa matstizo hsyo haujulikani ila baada labda kukabidhiwa Akili Mali , vinasema baadhi ya vikundi

    ReplyDelete
  2. Tumechoshwa nawimbo wa yanga mbona alivyokuepo lwandamila wachezaji hao ao ndio walikuwa wanapata matokeo.

    ReplyDelete
  3. Viongozi wa timu zetu waaachane na tabia ya kutafuta visingizio timu zinapofungwa. Wachezaji wanaosajiliwa na timu ni 30. wanaocheza 11. Sasa hao 7 muhimu ni vyuma au wanadamu? Ina maana wakiumwa timu isicheze? wengine sio wachezaji? Mbona akina Mateo,Martin, Buswita, Raphael Paul, Mahadhi, Muhilu ndio Kocha Lwandamila alikuwa akiwachezesha na wanafungia timu? Hebu tengenezeni kikosi kikali cha timu zetu za wachezaji 30 wote wawe muhimu na uwezo wa kuichezea timu. Tuachane na sababu Chirwa hakucheza ndio maana hatukufunga, Okwi na Bocco hawapo ndio maana timu imefungwa hizo sababu zimepitwa na wakati.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic