June 4, 2018


Vuguvugu la usajili kwa wachezaji wa soka nchini Tanzania linaendelea kama kawaida ambapo klabu ya Azam FC inatarajiwa kumtambulisha beki namba mbili wa Yanga, Juma Abdul.

Mchezaji awali alitakiwa kutambulishwa mbele ya Waandishi wa Habari wiki iliyopita lakini badala yake akatambulishwa kocha Hans van der Pluijm pekee.

Ofisa wa Habari wa Azam, Jaffar Maganga, mapema baada ya kumtangaza Plujim kuwa kocha wao mpya, alifunguka na kueleza Jumatatu itakuwa siku rasmi ya kulipua bomu jingine.

Endapo Abdul atatangazwa leo na Azam FC, atakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na Azam ndani ya mwaka huu baada ya Mzimambwe, Donald Ngoma.

Taarifa za chini zinaeleza tayari Azam wamemalizana na Ngoma na inaelezwa ameshaini mkataba wa miaka miwili.

3 COMMENTS:

  1. Yanga masikini imekuwa kama mbawala aliyezungukwa na kundi la fisi wenye njaa na imekuwa kila mmoja anabmega pande la nyama na kuondoka nalo. Msimba

    ReplyDelete
  2. Juma Abdul ni mchezaji mzuri lakini baada ya kupata injuries akarudi nyuma kidogo na Kessy akachukua namba moja kwa moja. Juma Abdul bado ni mzuri sana tu sasa afanyeje akipata nafasi Azam bora aende huko akacheze na pesa anapata ya uhakika.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic