Na Mwandishi Wetu, Nakuru
Kocha wa Simba, Pierre Lechantre amefunguka na kusema kwamba mshambuliaji wake mpya, Marcel Kaheza anapaswa ajitume la sivyo, nafasi itakuwa ngumu kwake.
Kocha huyo alimuingiza Kaheza katika dakika ya 45 katika mchezo wake wa kwanza wa Michuano ya SportPesa Super Cup kuchukua nafasi ya Mohamed Ibrahim, dakika ya 65 akamtoa nje.
Uamuzi huo ulionekana kuwachanganya wengi lakini baada ya mechi, Lechantre raia wa Ufaransa alisema hakuona alichokuwa akikifanya na kuamua kumuingiza Shiza Kichuya.
“Hakuwa akipambana, huu ni mfumo wangu. Haupambani, basi hakuna nafasi,” alisema.
Kaheza amerejea Simba akitokea Majimaji FC ambako alifunga mabao 14 ya Ligi Kuu Bara ingawa hayakuwa msaada kuibakiza timu hiyo Ligi Kuu Bara.
Kocha itakuwa kaona kitu kwa Kaheza na sio katika mtizamo hasi labda kama wengi wanaweza kufikiria bali mzazi mwenye mapemzi ya kweli na mwanae sie yule anaemuona mwanae anafanya mambo ya hovyo halafu akashindwa kumkemea kwakuwa anampenda hayo sio mapenzi bali ni maangamizi. Kaheza kama atajitunza vyema na kufuata maelekezo ya walimu wake basi kipindi si kirefu atatoka. Kaheza umri na umbo lake pamaoja na uwezo wake uwanjani vinavutia na ana kila sifa ya mshambuliaji wa kati isipokuwa tatizo la kaheza labda ni tatizo la vijana wetu wengi wa kitanzania nalo ni tatizo la kutojituma kwa kutojitolea muhanga kufanikisha malengo yao.
ReplyDeleteMchzaji anaejitambua hakuna siku rahisi na sherehe katika masaa yake ya kazi kama siku ya mechi. Kwanini? Jibu ni kwamba dakika za mchezo wa mpira ni 90 na ni wachezaji wachache wanaobahatika kukamilisha dakika tisini kila mechi. Sasa kama kweli mchezaji alikuwa akijituma kikamilifu kwenye mazoezi kwa takribani masaa mawili au matatu kimazoezi sasa kitu gani tena kitakachompelekea kuwa goigoi katika dakika tisini za mechi? Mazoezi hasa binafsi kwa kufuata taaluma ya mazoezi yanayoambatana na mlo wa malengo ndio siri ya akina Cristiano Ronaldo na wachezaji nyota wengine wengi Duniani . Watu watasema na kumsifia Ronaldo siku ya mechi e.. bwana we huyu Ronaldo achana nae kabisa,na hata yeye mwenyewe utamuona ana ringa ringa hivi na kutabasamu pale uwanjani siku ya mechi lakini nyuma ya pazia tayari alishajipitisha kwenye tanuri la moto katika siku zake za mazoezi kiasi cha mateso makubwa aliyoyakubali kuwa ndio rafiki yake mpendwa na pale uwanjani kaja kusheherekea mafanikio ya mazoezi kwa kufanya vitu anavyotaka kufanya kuwa rahisi na kumfanya kuwa bora.
Kutokuwa fiti ndicho kitu kinachoweza kumtia mchezaji pressure na mchecheto na si kitu kingine. Na Si kwa mwnamichezo tu hata mtu wa kawaida ukitaka kuwa na mwili utakaokufanya kufurahisha katika maisha yako basi fanya mazoezi wala usisubiri kwenda kupoteza pesa kwa mpiga tunguli kumbe tatizo ni kisukari.