Na Mwandishi Wetu, Nakuru
Baada ya Yanga kung’olewa katika mechi yao ya kwanza ya michuano ya Kombe la SportsPesa Super Cup, mashabiki wake waliamua kubaki mjini hapa, kushuhudia mechi kati ya Simba dhidi ya Kariobang Sharks.
Mashabiki hao wa Yanga ambao jana walishuhudia dakika 45, Yanga iking’olewa kwa kufungwa na Kakamega Homeboys, leo waligeuka mwiba kwa Simba.
Mashabiki hao muda mwingi walikuwa wakiwazomea wachezaji wa Simba na kuwashangilia Sharks.
Kipindi cha kwanza, Sharks waliwazidia Simba na kupoteza nafasi kadhaa za kufunga, kipa Aishi Manula akiwa shujaa.
Katika kipindi cha pili, Simba walibadilika lakini bado hawakuwa na madhara makubwa kwa Wakenya hao.
Wakati wa penalti, mashabiki hao walikuwa wakipiga kelele kutaka Manula aondoe taulo langoni mwake.
Duuuh!!!! Sasa huo ushari wa aina yake, kwani timu ya Simba ndo iliwatoa Yanga? Sasa wanafikiri ushabiki wa Tanzania ndo wanao wa Kenya. Sasa wamepata aibu kwao.
ReplyDeleteProtas-Iringa
Wamefungwa yanga na wataendelea kufungwa na kukimbiwa na wachezaji wao kutokana na ubaya na hasadi yao
ReplyDeleteMashabiki wa Yanga kupiga kambi Kenya ili kuzipa sapoti timu za Kenya zinapokutana na Simba kuhakikisha Simba inatolewa kwenye mashindano hayo. Sisi ni Watanzania hakuna cha ajabu ni watu wenye roho mbaya ya kutoona Mtanzania mwenzetu anafanakiwa.Wala usije ukapumbazika au kusikia vijisababu yakwamba ni ushabiki wa mpira kila mtu yupo huru kushabikia anapotaka, hapana bali Watanzania hivyo ndivyo tulivyo si kwenye mpira, SiaSa au kwenye burudani ni watu wenye roho mbaya,roho za husda. Huko kwenye Siasa ambako ndiko kunako hatma ya nchi yetu ndiko kumeoza kabisa. Kama uliwahi kusikia ndege ya Tanzania imezuiwa huko nje kwa fitna zilzotengenezwa na Watanzania wenyewe ili kuokomoa upande mwengine wa imani tofauti wa siasa ushindwe kufanikisha miradi ya maendeleo nchini ,sisi ni Watanzania bana. Manara licha ya mbwembwe zake zote kwa simba yake wakati mwengine kweli zinatia kichefuchefu kwa mashabiki wa timu pinzani lakini mapema kabisa wakati timu za Tanzania zinajiandaa katika mechi za kimataifa alishauri kuwe na uzalendo vilabu vyetu kwa mashabiki kuacha kushangilia timu ngeni timu zetu zinapocheza lakini Yanga kuanzia viongozi mpaka mashabiki walimchamba Haji Manara hadi aibu. Mwigulu Mchemba ni shabiki au miongoni mwa viongozi walezi wa Yanga na kutokana na majukumu yake ya kazi serikalini kuwa mazito anatakiwa kufahamu yakuwa Watanzania wanamatatizo ya uzalendo na Taifa ambalo wananchi wake wamekosa uzalendo huwa umeliweka suala lake la usalama rehani kwa maadui wa nje na wa ndani na hata kusimama kwake kama Taifa kutakuwa na mashaka. Na kama hiyo haitoshi timu yake anayoishabikia ndio chanzo cha ukosefu wa uzalendo linapokuja suala la kuzisapoti timu zetu zinapocheza na timu za nje sasa ipo haja sisi kama Watanzania kujitafakari upya la sivyo hatutafika popote kwa jambo lolote lile.
ReplyDeleteKweli nakubali sasa kuwa tuna roho za chuki na ni wapuuzi
ReplyDeleteMwandishi ulikosa cha kuandika????? Huu uandishi ni wa uchochezi
ReplyDeleteSio uchochezi ni vizuri lakini aibu zaidi kwa yanga hata huko ugenini kuonesha uovu na ilibidi kwanza wajihurumie kwa mambo yanavowaendea kabla ya kuwaombea wengine maovu. Kwa roho hiyo hawajui kuwa Mungu hatawabariki mpaka kwanza wasafishe nyoyo?
ReplyDelete