June 8, 2018


Na George Mganga

Kocha Msaidizi wa Simba, Masoud Djuma, amekabidhiwa majukumu yote ya Mfaransa Pierre Lechantre kwa kipindi hiki baada ya kuondoka Kenya na kuiacha timu ikijiandaa na fainali ya mashindano ya Super CUP dhidi ya Gor Mahia FC.

Mrundi huyo ataingoza Simba kucheza fainali ya Super CUP dhidi ya Gor Mahia Jumapili ya wiki hii kwenye Uwanja wa Afraha akiwa Kocha pekee kwenye benchi la ufundi la timu hiyo.

Lechantre pamoja na Mwalimu wa viungo, Aimen Habib wameondoka leo asubuhi kurejea Tanzania kwa ajili ya kujua hatima ya mikataba yao ambayo inamalizika siku kadhaa zilizosalia.

Kuondoka kwao Mfaransa huyo kunampa majukumu yote Djuma kuiandaa timu kuelekea mchezo wa fainali hiyo ambapo kikosi kitakuwa chini yake mpaka mwisho wa mashindano.

Kocha Djuma amekuwa akililiwa na mashabiki wengi wa Simba kwa muda mrefu wakiomba akabidhiwe timu huku wakiuomba uongozi umtimue Mfaransa Lechantre wakidai kutoridhishwa na kiwango cha timu ikiwa chini yake.

Haijajulikana baada ya mashindano ya Super Cup kama uongozi wa Simba utampa Djuma majukumu ya kuwa Kocha Mkuu ama utamsajili mwingine, pengine tusubiri kuona itakuwaje.

Lechantre alikuja Simba kuchukua nafasi ya Mcameroon Joseph Omog, aliyetumuliwa mapema baada ya kupoteza mchezo wa FA dhidi ya Green Warriors na kusaini mkataba wa miezi sita.

1 COMMENTS:

  1. Ushauri wangu kwa Uongozi wa SIMBA: Djuma apewe ukocha mkuu. Anastahili. Mvumilivu na anajua kazi yake. Achaneni na wazungu hawa. Djuma hata wachezaji wako karibu naye. Djuma hapaki bus. Wachezaji wanatafuta magoli sio kupaki gari. Mpeni Djuma ukocha Mkuu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic