June 15, 2018



Yanga inaonekana kuvutiwa na mshambuliaji Meddy Kagere wa Gor Mahia, lakini sasa matumaini ya kumpata yanaonekana kuyayuka.

Maana Kocha Mkuu wa Gor Mahia, Dylan Kerr, amesema amekuwa akishangazwa na taarifa za kuwa mshambuliaji wake, Meddy Kagere anatarajia kujiunga na Yanga.

Kerr amesema Kagere ambaye ni mfungaji bora wa michuano ya SportPesa Super Cup hatakwenda popote.

Kumekuwa na taarifa kwamba Yanga inafanya kila njia kumpata Kagere.

 Kerr, raia wa Uingereza, amefunguka kuhusiana na Kagere na kusema, Yanga wasahau.

“Nimesikia sana, lakini Kagere hatakwenda popote, acha tu waendelee kusema,”  alisema.
Hata hivyo, Kerr hakutaka kufafanua kwa nini mshambulizi wake huyo hatakwenda popote.

Taarifa zinaeleza, Kagere bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Gor Mahia.

Taarifa nyingine zinaeleza, Kagere amefanya mazungumzo ya kuongeza mkataba na klabu yake ya Gor Mahia.

Lakini mmoja wa rafiki zake ameliambia gazeti hili kwamba kuna ugumu Kagere kwenda Yanga kama inavyoelezwa kwa kuwa ana ushindani mkubwa wa namba na Jacques Tuyisenge.

“Yeye na Tuyisenge wanacheza namba moja timu ya taifa ya Rwanda. Anajua Yanga hawachezi michuano ya kimataifa, akiondoka Gor ni sawa na kujiondoa Amavubi,” alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic