June 9, 2018


Ni rasmi sasa Kocha wa Simba, Mfaransa, Pierre Lechantre, ametimuliwa Msimbazi. Hii ni baada ya Championi kunasa taarifa hizo takriban wiki mbili kabla.

Lechantre, ambaye alitua Simba Januari, mwaka huu na kuanza mechi yake ya kwanza Januari 28, ametimuliwa baada ya kuiongoza Simba kwa mechi 15 tu za Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kisa kikubwa cha kutimuliwa kama ilivyoandikwa katika gazeti bora la michezo Tanzania, Championi, ni madai yake ya mshahara wa Sh milioni 90 kila mwezi ili asaini mkataba mpya.

Pamoja na sababu hiyo, Lechantre ambaye alikwenda Kenya kuiongoza Simba katika michuano ya SportPesa Super Cup, jana kabla ya mchezo wa nusu fainali dhidi ya Kakamega Home Boys, kocha huyo aligoma kuiongoza timu akidai mkataba mpya.


Taarifa kwa mujibu wa gazeti la Championi zinaeleza kwamba, Lechantre aliondoka Bongo akiwa amekubaliana na mwekezaji wa Simba, Mohamed Dewji ‘Mo’ kuwa atapewa mkataba baada ya kumalizika kwa michuano ya SportPesa Super Cup.

Lakini jana, alipomuona Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’, alimlalamikia kuwa hana mkataba na akadai hawezi kuendelea kuiongoza timu hiyo akiwa hana mkataba.

Baada ya mabishano ya muda mrefu, Try Again alikubali kwamba asiiongoze Simba jana dhidi ya Kakamega, na badala yake Mfaransa huyo akaenda kukaa jukwaani na mashabiki akiwa amenuna, huku msaidizi wake Masoud Djuma akiiongoza Simba kutinga fainali kwa mikwaju ya penalty 5-4.

Baada ya kugoma kuiongoza timu hiyo jana, ndipo ikaelezwa kuwa Try Again akachukua uamuzi wa kumng’oa rasmi Mfaransa huyo ambaye ameiongoza Simba kubeba ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2017/18, akichukua mikoba ya Mcameroon, Joseph Omog ambaye alimaliza mzunguko wa kwanza akiwa hajapoteza mechi yoyote.

3 COMMENTS:

  1. afadhali,hajafanya kitu zaidi ya kutumia falsafa za irambona.nadhani pia sio mzuri kwenye malezi ya wachezaji.alijiweka kama boss wakati kuilea timu inataka friendship.

    ReplyDelete
  2. afadhali,hajafanya kitu zaidi ya kutumia falsafa za irambona.nadhani pia sio mzuri kwenye malezi ya wachezaji.alijiweka kama boss wakati kuilea timu inataka friendship.

    ReplyDelete
  3. Maamuzi mazuri hakuwa kocha mzuri alitamani pesa ndefu sana kwa klabu zetu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic