June 9, 2018



Mshambuliaji mpya wa Azam FC, Donald Ngoma, anawasili leo nchini akitokea Afrika Kusini alipokuwa amepelekwa kufanyiwa vipimo vya afya.

Ngoma alikuwa katika jiji la Cape Town kwa ajili ya vipimo hivyo ambavyo tayari vimekamilika na leo mchana Daktari wake atatoa ripoti ya matokeo ya vipimo hivyo.

Kwa mujibu wa Afisa Habari wa klabu ya Azam, Jaffer Idd, amesema Ngoma atawasili majira ya leo mchana akiwa sambamba na daktrari wake aliyeenda naye Afrika Kusini.

Ikimbukwe Ngoma alishindwa kucheza talribani mechi zote za msimu uliopita kutokana na kusumbuliwa na majeraha wakati akiwa Yanga.

Mapema baada ya kuingia naye mkataba, Azam waliazimia kumsafirisha mpaka Cape Town kwa ajili ya kufanyiwa vipimo kiafya.

2 COMMENTS:

  1. Samaki akioza usimtupe umtafutie viungo umkaushe atakuja kumuokota mwenzio ulie uje ujute. Walisema wa zamani

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kweli km Tambwe alivyitupwa Yanga wakamuokota.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic