June 7, 2018


Na George Mganga

Kocha Mkuu wa Simba, Mfaransa Pierre Lechantre pamoja na Mwalimu wa viungo, Aimen Habib, kwa pamoja watakosekana katika benchi la ufundi wakati Simba ikicheza dhidi ya Kakamega HomeBoyz FC leo.


Katika orodha ya wachezaji na benchi la ufundi wa kikosi hicho iliyotoka punde inaonesha Kocha Msaidizi pekee, Masoud Djuma ndiye atakuwa anaiongoza Simba katika mchezo wa nusu fainali ya Super Cup huko Kenya.


Haijajulikana sababu ya za kukosekana kwa wawili hao ni zipi ingawa imekuwa ikielezwa wamekuwa hawana mahusiano mazuri na kocha Msaidizi wa kikosi hizho.


Hivi karibuni kumezuka taarifa zinazoeleza kuwa Lechantre anaweza akatimkia Cameroon kwa ajili ya kutegemea kibarua cha kuinoa timu ya taifa hilo baada ya kutuma maombi ya kuomba kazi.


Aidha taarifa za ndani pia zinaeleza Lechantre na Aimen inawezekana safari ya kuitumikia Simba inaweza ikaishia baada ya michuano ya Super Cup kumalizika.

2 COMMENTS:

  1. Sawa hawana lao jambo. Wamefika wameikuta Simba imeshakata mbuga kuelekea kilele cha mafanikio na tulichoshuhudia timu kukosa speed na maamuzi ya kubomoa wala sio ya kujenga

    ReplyDelete
  2. Kwa faida ya timu ni bora waondoke. Djuma anatosha

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV