June 13, 2018


Winga wa klabu ya Yanga, Geoffrey Mwashiuya amekuwa chachu ya mashabiki katika mashindano ya ligi ya Kimondo Day inayoendela katika mkoa wa Songwe akiwa na timu ya Hazundila FC.

Mchezaji huyo anaitumia likoz yake katika ligi hiyo baada ya uongozi wa Yanga kutoa mapumziko kwa wachezaji wake kabla ya kurejea kujiandaa na mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gor Mahia ya Kenya.

Mwashiuya alikiongoza kikosi chake kuibuka na ushindi wa mabao yaliyopatikana kwa changamoto ya matuta 9-8 baada ya dakika 90 kwenda sare tasa ya 0-0 dhidi ya Tunduma City kwenye Uwanja wa CCM Vwawa mjini Mbozi.

Taarifa zinaeleza kuwa Mwahiuya ameyafurahia mashindano hayo yanaendelea mjini humo kutokana na namna yanavyoibua vipaji vya vijana wengi ambao wanapenda mchezo wa soka.

Winga huyo atarejea kambini wiki ijayo kujiunga na wachezaji wenzake kwenye kikosi cha Yanga kwa ajili ya kuanza maandalizi ya dozi dhidi ya Gor Mahia FC.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic