June 11, 2018


Wanachama wa klabu ya Yanga leo hii wamepinga hatua kujiuzulu kwa aliyekuwa mwenyekiti wa klabu hiyo, Yusuf Manji katika mkutano mkuu wa klabu hiyo uliyofanyika kwenye Ukumbi wa Maofisa wa Polisi, Oyster Bay jijini Dar es Salaam.

Zaidi ya wanachama 1,400 waliohudhuria mkutano huo wamedai kuwa Manji bao ni mwenyekiti wao mpaka mwaka 2020 ambapo muda wake wa utawala klabuni hapo utakapokoma kwa mujibu wa katiba ya klabu hiyo.

Hivi karibuni Manji aliandika barua ya kujiuzulu nafasi yake ya uenyekiti wa klabu hiyo ili akapumzike,  jambo ambalo liliwashitua na kuwaumiza wanachama na wapenzi wa klabu hiyo.

Katika hatua nyingine, wanachama wa klabu hiyo kwa pamoja wameridhia kufanya mabadiliko ya mfumo wa uendeshwaji wa klabu hiyo.

Kwa pamoja wamepaza sauti zao na kutaka kuondokana na mfumo wa sasa wa uanachama na kuingia katika ule wa hisa kama ilivyofanya klabu ya Simba hivi karibuni.

Pia katika mkutano huyo ambao ulifunguliwa na Wazira Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe, wanachama hao wameridhia mapendekezo ya uongozi wa klabu hiyo ya kuunda kamati mpya itakayosimamia masuala yote ya usajili wa timu hiyo.

Kamati hiyo yenye wajumbe tisa, itaongozwa na aliyewahi kuwa mwenyekiti klabu hiyo, Abbas Tarimba,  akisaidiana aliyekuwa mkuu wa mkoa wa zamani wa Dar es Salaam na Kilimanjaro, Said Meck Sadick.

1 COMMENTS:

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV