June 17, 2018


Na George Mganga

Hatua ya robo fainali ya michuano ya Uhai CUP (U20) inaendelea tena leo kwenye Uwanja wa Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) kwa mechi mbili kutimua vumbi.

Stand United kutoka Shinyanga itakuwa inacheza na Ndanda FC ya Mtwara, mchezo utakaoanza majira ya saa 8 mchana.

Wakati huo Simba ambao ni mabingwa watetezi watakuwa kibaruani kukipiga na Tanzania Prisons ya Mbeya kuanzia saa 10 kamili jioni.

Mechi hizo zinaendelea ikiwa ni baada ya jana Azam na Mtibwa Sugar kufuzu kuingia nusu fainali.

Azam ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbao FC halikadhalika Mtibwa ikiifunga Ruvu Shooting 1-0.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic