June 17, 2018


Na George Mganga

Wakati presha ya usajili wa wachezaji wapya kwa klabu za hapa Tanzania ukiendelea kushika kasi, Mwenyekiti wa Kamati Maluum ya kuivusha Yanga wakati wa mpito, Abass Tarimba, amesema jukumu kubwa la Kamati hiyo ni kushauri.

Tarimba ameeleza kazi hiyo wanaifanya kwa kushirikiana na Kamati ya Utendani ndani ya klabu pamoja na ile ya usajili ili kuhakikisha mipango yote inaenda sawa.

Mwenyekiti huyo ameeleza kwa sasa watakuwa wanafukuza mwizi kimyakimya na hawatoweza wazi kiasi cha miamala yao yote itakayokuwa inafanyika.

Tarimba amesema wataenda kimyakimya kutokna na matamko ya uongozi wa klabu hiyo hivi karibuni wamekuwa wakikataa kutaja wachezaji walio kwenye mipango yao ya kuwasajili sababu wamekuwa wakisajiliwa na timu zingine.

"Kamati yetu sisi ni ya ushauri, ni kamati ambayo imepewa mamlaka hayo kupitia Mkutano Mkuu uliofanyika, lengo letu itakuwa ni kumfukuza mwizi kimyakimya, hatutakuwa tunatangaza wazi miamala itakayokuwa inafanyika" alisema.

Kwa mujibu wa Tarimba ameahidi kamati yao kutekeleza kazi yao hiyo maalum pamoja na kuwa sehemu ya ushauri kwa viongozi wa Yanga kupitia Kamati ya Utendaji na Usajili.

3 COMMENTS:

  1. Ushauri wangu kwa Mheshimiwa Tarimba, lipo tatizo la uwepo wako kwenye Sportpesa kunaweza kuwepo mgongano wa kimaslahi. Achia kimojawapo.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Shughuli hazifanani hata kidogo, ni sawa kumwambia Nassoro Idrissa Wa Azam aitoe Azam kwenye ligi kwa kuwa kampuni yao inadhamini ligi.

      Delete
    2. Shughuli hazifanani hata kidogo, ni sawa kumwambia Nassoro Idrissa Wa Azam aitoe Azam kwenye ligi kwa kuwa kampuni yao inadhamini ligi.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic