Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), wakishirikiana na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), jana limezindua rasmi mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kagame) yanayotarajiwa kuanza Juni 29, mwaka huu huku Simba na Yanga zikipangwa kwenye kundi moja.
Hii ni rekodi mpya kwa michuano yote ambayo imekuwa ikiandaliwa kwenye ukanda huu ambapo hakuna kipindi huku nyuma ambacho timu hizo zimewahi kuwekwa kundi moja.
Hata hivyo, pamoja na kwamba timu hizo zimepangwa kundi moja, kuna uwezekano mkubwa zikakutana tena kwenye hatua za mbele aidha fainali au mshindi wa tatu kama zote zitapenya hali ambayo inaonyesha kuwa kuna uwezekano timu hizo zikavaana mara mbili ndani ya mwezi mmoja jambo ambalo pia ni rekodi.
Katika mashindano hayo yatakayoshirikisha timu 12 ambapo Kundi A kuna Azam ya Tanzania, Resps (Uganda), JKU (Zanzibar), Kator (Sudani ya Kusini) na Kund B, Rayon Sport (Rwanda), Gor Mahia (Kenya), Lydia Ludic (Burundi) na Ports Djibouti wakati Kundi C kuna Simba, Yanga zote za Tanzania, St George kutoka Ethiopia na Dakadaha ya Somalia.
Kuelekea mashindnao hayo, Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholas Musonye, alisema kuwa kwa upande wao wana furaha kubwa mashindano hayo kufanyika tena hapa nchini baada ya kupitia miaka miwili iliyokuwa na changamoto nyingi huku akiwatambulisha Azam TV, kama wadhamini wa mashindano hayo.
Katika hatua nyingine, bingwa wa michuano hiyo atapata zawadi za Dola za Marekani 30,000 (Sh milioni 60), mshindi wa pili Dola za Marekani 20,000 (Sh milioni 40) na mshindi wa tatu Dola za Marekani 10,000 (Sh milioni 20)..
0 COMMENTS:
Post a Comment