PICHAZ: SIMBA YAFUZU KUINGIA NUSU FAINALI SPORTPESA CUP, YAIONDOA KARIOBANGI KWA MATUTA
Na George Mganga
Kikosi cha Simba kimefanikiwa kusonga mbele mpaka hatua ya nusu fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup kwa ushindi wa matuta 3-2 dhidi ya Kariobang Sharks ya Kenya.
Mchezo uliokuwa uanpigwa Uwanja wa Afraha, umeshuhudiwa ukimalizika ndani ya dakika 90 huku kila timu ikishindwa kuona lango la timu pinzani.
Baada ya dakika 90 kumalizika hatua ya upigaji wa matuta ulifuatia na Simba ikaweza kupata penati mbili zilizofungwa na Erasto Nyoni, Haruna Niyonzima na Jonas Mkude.
Matokeo hayo yanaifanya Simba kuwa timu ya kwanza kuingia nusu fainali baada ya Yanga na JKU zote kutolewa jana.
Baada ya Simba kuvuka robo fainali leo, Tanzania itawakilishwa tena na Singida United kesho katika Uwanja huohuo wa Afraha.
Hongera Simba kwa kusonga mbele ila Timu inayokuja mbele ni Ngumu zaidi ni wale wababe wa Yanga kwa hivyo umakini unahitajika zaidi. Ni wakati wa Simba kuwalipia kisasi Yanga kwa Kakamega home boys.
ReplyDeleteMashindano haya kwa timu za Kenya Piga ua,karagaza wanachofikiria ni kwenda Uiengeza kucheza na Everton hakuna kingine kwa hivyo kila timu shiriki kutoka Kenya katika mashindano haya wamejipnga hasa.
Kariobangi Sharks ni timu ya 5 mpaka sasa kwenye ligi ya Kenya.KK homeboys ni ya 9 mpaka sasa kwenye ligi.Pia timu za Kenya zina advantage ligi yao bado inaendelea hivyo wako fiti zaidi ya timu zetu zilizomaliza ligi .
ReplyDeleteKila la heri timu ya Simba kwa hatua ambayo mmefikia hadi sasa
ReplyDeleteProtas-Iringa
Aibu kubwaa.mshabiki wa yanga ugenini waizomea Simba kuishangilia Sharks. Munhu alikuwa pamoja na Simmba ambae kashinda na yanga ikigaragazwa kwa kuchapwa tatu.Wanazi kujiangamiza na kila wanapokwenda vichapo.
ReplyDeleteWanachofanya shabiki wa Yanga huko Kenya kwa ss ni kujiaibisha wenyewe na kutuaibisha watanzania. Wanachokifanya ni aibu tupu. Bora wakae tu bila kushangilia au waijindoe huko warudi haya mambo yafanyike humu kwetu na sio ugenini. Kwa wenzetu hii ni Story kuu kwenye medias zao.
DeleteWana matatizo akilini
ReplyDelete