June 8, 2018


Na George Mganga

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limethibitisha kupokea barua ya Yanga yenye ombi la kujiondoa kwenye mashindano ya Kagame Cup yanayotarajia kuanza Juni 29 mpaka Julai 13 2018.

Kwa mujibu wa Ofisa wa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo, amesema wamepokea barua hiyo inayoeleza kuwa Yanga ina nia ya kuwapa mapumziko wachezaji wake.

Barua hiyo iliyowasili katika makao makuu ya TFF, imesema Yanga inahitaji kuwapa muda wa kupumzika wachezaji wake kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga itakuwa ina kibarua kizito kitakachopigwa nchini Kenya dhidi ya mabingwa wa ligi nchini humo kwa msimu wa 2017/18, Gor Mahia FC Julai 18.

Kutokana na muingiliano wa ratiba hiyo ya Kagame na CAF, Yanga wameona ni vema zaidi kuwapa wachezaji wake mapumziko ili kujiandaa kuelekea mechi hiyo ya kimataifa.

7 COMMENTS:

  1. Watched longolongo na kuwa wawazi. Sababu kubwa ni kutokana na kupangwa kundi moja na simba. Wamekwepa sportspesa super cup Huko Kenya baada ya kubaini kuwa Kama angeshinda mechi yake ya kwanza, inayofuatia ilikuwa akutane na mnyama

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kweli Yanga hawana akili.. Hilo kombe la Shirikisho wanalojiandaa nalo wanasindikiza tu. Ni bora wangecheza hata hiyo Kagame. Kweli Yanga mtarudi kwenye form miaka 30 ijayo

      Delete
  2. Ikiwa hofu yao kuwekwa kundi moja na Simba kama ilivotokea
    miaka ya nyuma na kupambana na adhabu kali ambapo huenda hilo likatokea tena, basi wangelijaribu kuomba kuwekwa katika kundi jengine na sababu zao walixozitoa ni chapwa na hazina msingi. Ikiwa wao sababu wanasema kuwa wanajitayarisha na mechi yao na Gormahia, basi mechi hizo za Kagame si zingewasaidia kujipima walipofika au hawatohitaji kujipima wana uhakika na ushindi. Kujitoa kwao inatokana na vitisho vya Haji Manara hivi karibuni pale alipoomba duwa wakutane tena na Yanga ndio hapo wakapanda kihoro. Jee hawaogopi adhabu ya TFF au ndio lengo lao ili waikimbie na Gormahia? Msiba si mdogo

    ReplyDelete
  3. Nina mashaka na viongozi wa Yanga kuhusu weledi, fikra, maamuzi wanayoyafanya, sina uhakika kama wamepata elimu sahihi ya kuchanganua hoja na kutoa maamuzi yenye utashi na mashiko....hii inaonyesha taswira ya viongozi tulionao na ambao tunawachagua katika kamati za usajili, mashindano nk. Sababu zilizotolewa hazina mashiko mbona Rayon FC, Gor Mahia ambao wao tena bado wako kwenye ligi na mashindano ya CAF na sportspesa hawajaandika barua kujitoa?

    ReplyDelete
  4. Hahahahaaaa Mpira bongo Bado Sana, Sisi komedi na masihara ndio zetu

    ReplyDelete
  5. Yaani Baada ya kukimbizwa vilivyo na kakamega Jamaa wameomba Likizo ya mapumziko. Sasa wakicheza na Gor sijui wataomba nn Hahahahaaaa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic