YAJUE MAMBO MAKUBWA MATANO YALIYOJITOKEZA KOMBE LA DUNIA URUSI TANGU KUZINDULIWA KWAKE JUNI 14 2018
Na George Mganga
Wakati mitanange minne ikitarajiwa kupigwa leo katika mwendelezo wa michuano ya Kombe la Dunia huko Urusi, haya hapa mambo matano makubwa yaliyojitokeza tangu kuzinduliwa rasmi kwa mashindano hayo juzi.
Timu pekee za Afrika ambazo ni Misri na Morocco zimeweza kupoteza mechi zao za kwanza katika dakika za mwisho, zote zimefungwa bao 1-0. Misri imepoteza dhidi ya Uruguay na Morocco ikafungwa na Iran.
Nyota anayekipiga katika klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo, amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao matatu pekee ndani ya mchezo mmoja (Hat-Trick) ikiwa dhidi ya Spain. Mechi hiyo ilimalizika kwa matokeo ya sare ya mabao 3-3.
Wakati Nigeria wakijiandaa kutupa karata yao ya kwanza leo dhidi ya Croatia, vigogo hao wa soka barani Afrika wameshinda jumla ya mechi 5 dhidi ya timu za mataifa ya Ulaya huku wakienda sare 1 na kupoteza pia mechi 5 tangu kuanzishwa kwa michuano hiyo.
Timu za Morocco na Iran zimekutana jana kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa michuano hiyo mikubwa ikiwa ni katika mchezo wa kundi B na Iran kuibuka na ushindi wa bao 1-0.
Nyota wa Misri, Mohamed Salah ameweka rekodi ya aina yake baada ya kushuhudia timu yake ikicheza mchezo wa kwanza na kupoteza dhidi ya Uruguay kwa bao 1-0 huku akiwa benchi na ikiwa ni siku yake maalum ya kuzaliwa. Alizaliwa Juni 15 1992 (Miaka 26).
0 COMMENTS:
Post a Comment