June 16, 2018


Hassan Kessy ambaye anacheza nafasi ya beki ya pembeni kwenye kikosi cha Yanga, amesema yupo tayari kuendelea kuvaa jezi msimu ujao ikiwa tu atapewa dau la Sh mil 60.

Beki huyo ni kati ya wachezaji 11 muhimu katika timu ambao mikataba yao imemalizika mwishoni mwa msimu uliomalizika wa Ligi Kuu Bara.

Wachezaji wengine ni Obrey Chirwa, Kelvin Yondani, Beno Kakolanya, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Said Makapu na Andrew Vicent ‘Dante’.

Kessy ambaye alijiunga na Yanga misimu mawili iliyopita akitokea Simba SC, ameliambia Championi Jumamosi kuwa, maslahi pekee ndiyo yatakayombakiza Yanga ambayo dau la usajili na mshahara wa kila mwezi kwa kipindi ambacho atakachokuwepo Jangwani.

“Kila mtu aliona mchango wangu nilioutoa katika timu kwenye msimu uliopita wa ligi kwa kufanikiwa kuipambania timu na kuifikisha katika nafasi nzuri ya tatu tukiwa katika hali mbaya ya kiuchumi.

“Hivyo, nitakubali kubaki Yanga kwa dau hilo la usajili ambalo nimewapa mabosi wangu na pia kuangalia maboresho ya mshahara wangu mpya.

“Tofauti na Yanga, pia nipo kwenye mazungumzo na baadhi ya klabu za hapa nchini na nje ya nchi ambayo ni Motema Pembe (ya DR Congo) iliyoonyesha nia kubwa ya kunihitaji,” alisema Kessy ambaye aliwahi kuichezea Simba tena akaachana nao kwa mbinde.

Mmoja wa viongozi wa kamati ya muda ya Yanga alipodokezwa jana kuhusiana na ishu hiyo ya Kessy alidai kwamba hayo ni maneno wakikutana watayajenga.

CHANZO: CHAMPIONI

2 COMMENTS:

  1. Yanga mpeni sh 40 milioni atakubali tu kuitumikia Yanga hana popote pa kwenda labda Mbeya City. Timu za Simba na Azam hawawezi kumchukua huyo mchezaji.

    ReplyDelete
  2. Wampe milion 10 itapendeza zaidi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic