YANGA KUREJEA LEO JIJINI DAR ES SALAAM
Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuanza safari ya kurejea leo jijini Dar es Salaam kikitokea Kenya ambako kilienda kushiriki mashindano ya SportPesa Super Cup.
Yanga imeshindwa kuendelea na mashindano baada ya kutolewa katika mechi ya kwanza ikikubali kufungwa mabao 3-1 na Kakamega HomeBoys.
Yanga imepoteza mchezo huo ikiwa ni mwendelezo mbaya wa matokeo hasi tangu aliyekuwa kocha wake, Mzambia, George Lwandamina aondoke kuelekea kwao.
Ukiachana na Yanga, JKU ya Zanzibar nayo inatarajiwa kuwasili leo nchini baada ya kutolewa pia na Gor Mahia kwa idaidi ya mabao 3-0.
Simba SC na Singida United ndizo timu pekee zilizosalia kwenye mashindano hayo kwa sasa.
Baada ya kurejea nchini, taarifa zinaeleza kuwa Yanga itaanza maaandalizi mengine ya kujiwinda kucheza na Gor Mahia FC kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika mwezi ujao.
Wanafika na ndege gani Kenya Airways? Saa ngapi tukaipokee timu?
ReplyDeleteJee na wale walokwenda specialkuwapa sapoti sharks na kuwazomea Bingwa Simba alieshinda katika mechi yake nao watarejea kini au bado watabaki kuizpmea tena Simba katika half final ijayo?, Hawa jamaa hawajui aibu na wala hawaoni haya hata ugenini
ReplyDelete