SINGIDA UNITED WATOA SABABU ZA KUMUACHIA KUTINYU, WAELEZA KUWA PESA NI MUHIMU
Mkurugenzi wa klabu ya Singida United, Festo Sanga, ameibuka na kuweka wazi sababu ya kumuachia nyota wake, Mzimbabwe, Tafadzwa Kutinyu, aliyefanya vizuri msimu uliopita ndani ya kikosi chao.
Sanga ameeleza kuwa Singida ni klabu ya biashara hivyo linapotokea dau la fedha nono kutka upande wa pili wako tayari kumuuza kisha wataziba pengo lake.
Sanga amesema hawajaona tatizo kuuachia nyota huyo kwani tayari wameshapata wa kuziba pengo lake kutokana na usajili ambao wameufanya na wataendelea kusajili wengine.
"Unajua Singida United ni klabu ya kibiashara, kama timu imekuja mezani na fedha nzuri ikimtaka mchezaji, tuko tayari kuuza" alisema.
Singida United imemuachia nyota wake, Kutinyu ambaye ameelekea Azam FC kuungana na Kocha Hans van der Pluijm aliyesaini mkataba wa miaka miwili.
Ni sawa kufanya biashara ya kuuza wachezaji lakini viongozi mchukue tahadhali kubwa. Simba SC imeporomoka baada ya kuchukua ubingwa mwaka 2012/13 kwa sera hiyohiyo mbovu ya kudhani una kisima cha wachezaji wazuri unauza mastaa wako. Rage ndio ilikuwa sera yake na akaiingiza timu kwenye msongo wa miaka mitano ya kutafuta ubingwa kwa tochi. Faida ya zile pesa ni ndogo ukifananisha na gharama na hasara na kero ya kuutafuta tena ubingwa huo. Lazima mjifunze kwa waliokosea. Sio kila mchezaji atakuwa Okwi au Boko au Chirwa au Ngoma. Kichuya huwezi kutaka kumuuza kisa timu imeleta mezani sh 50m. Wapo wachezaji ambao hupaswi kufikiria kuwauza kirahisirahisi.
ReplyDelete