June 19, 2018




Wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya kimataifa, Yanga wataanza mazoezi Jumatatu ijayo tayari kuivaa Gor Mahia ya Kenya.

Yanga wataanza mazoezi ikiwa ni siku mbili baada ya kurejea kwa Kocha wao, Mwinyi Zahera aliyekuwa kwao DR Congo.

Meneja wa Yanga, Hafidhi Saleh amesema wataanza maandalizi Jumatatu kwa ajili ya mechi hiyo ya kimataifa.

“Jumatatu ndiyo siku rasmi, kwanza tutaanza off camp (kambi ya kwenda na kurudi), baada ya hapo litakuwa ni suala la mwalimu na uongozi nini kinafuatia,” alisema.

Yanga inajiandaa kucheza mechi yake ya tatu ya Kombe la Shirikisho hatua ya makundi itakayopigwa jijini Nairobi Juni 18.

Katika mechi ya kwanza, Yanga ilipoteza mechi yake ya kwanza ugenini Algeria kabla ya kutoka sare dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda jijini Dar es Salaam.

2 COMMENTS:

  1. Najiuliza tu.. timu yangu ya Yanga ina wachezaji saba tu wenye mikataba je ndio hao watakao anza mazoezi? Au ndio vile tutaendelea kuwatumia vijana wale waliomalizia mechi za ligi kuu? najiuliza tu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic