September 21, 2021

 


UONGOZI wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) umeweka wazi kuwa maandalizi kuelekea mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Simba v Yanga yamekamilika na matumaini yao makubwa ni kuona kwamba mchezo huo utaandika rekodi mpya ya ubora wa maandalizi yake.

Simba na Yanga zinatarajiwa kukutana Jumamosi ya Septemba 25, katika mchezo wa kukata na shoka utakaochoezwa Uwanja wa Mkapa.

Ikumbukwe kwamba mchezo wa Ngao ya Jamii ni maalumu kwa ajili ya kutoa taarifa kwamba pazia la Ligi Kuu Bara kwa msimu mpya linafunguliwa na ratiba ipo tayari kwa msimu wa 2021/22.

Mkuu wa Idara ya Ligi, Jonathan Kassano amesema kuwa kila kitu kuhusiana na mchezo huo kipo sawa na kinachosubiriwa ni mchezo wenyewe.

"Kila kitu kuhusiana na maandalizi ya mchezo wa Ngao ya Jamii ambao unatarajia kuzikutanisha Simba na Yanga utakaochezwa Uwanja wa Mkapa kimekamilika na kinachosubiriwa niJumamosi ifike utekelezaji wa mchezo huo.

"Kutokana na maandalizi ambayo tumeyafanya mpaka sasa tunaamini kwamba mchezo wa mwaka huu utaweka rekodi ambayo haikuwahi kuandikwa katika maandalizi ya mchezo huo," amesema.

Chanzo:Championi.

2 COMMENTS:

  1. kwanza ilibidi wacheze simba A na simba B, mabingwa wa vpl na FA sasa hao yanga wanabebwa hata ngao ya jamii?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic