BAADA YA DAU LA MILIONI 70 KUFELI, KESSY ATAKA KIASI HIKI CHA FEDHA NA NDINGA ILI ASAINI YANGA
Imeelezwa kuwa beki wa kulia aliyemaliza mkataba na klabu ya Yanga, Hassan Kessy amewarahishia kazi mabosi wake kwa kushusha kiasi cha dau la milioni 70 ili aongeze mkataba mpya.
Kessy alitaja dau hilo mwanzoni lakini sasa ameshusha kwa kukata kiasi cha milioni 20 na kubaki 50 pamoja na gari ili kusaini mkataba mpya.
Beki huyo ameeleza kuwa bado anatamani kuendelea kuichezea Yanga na mpira ni sehemu ya maisha yake hivyo ni vema Yanga wakampa gari na milino 50 za kitanzania ili aendelee kuwa na timu hiyo.
Kitita cha milioni 70 za mwanzo kiliwapa mzigo mkubwa Yanga kutokana na timu kuwa na wakati mgumu hivi sasa baada ya kukumbwa na uhaba wa fedha hivyo uliowafanya kushindwa kumpa Kessy kiasi hicho cha fedha.
Baada ya kupunguza mpaka milioni 50, inawezekana Yanga sasa wakajipanga upya kwa ajili ya kumalizana naye tayari kuanza safari ya kukijenga vizuri kikosi hicho kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.








This comment has been removed by the author.
ReplyDeleteYanga hawana hiyo milioni 50 ya kumpa Kessy, labda Kessy asaini kwa mali kauli.. Namshauri Hassan Kessy asione aibu bali arudi Mtwibwa Sugar
ReplyDeleteKwel mbona mwenzake juma luzio amerud afanye haraka
ReplyDelete