July 15, 2018


Na George Mganga

Baada ya kuondokewa na wachezaji wake tegemeo, uongozi wa klabu ya mtibwa Sugar umefunguka na kueleza kuwa sasa watakiboresha upya kikosi chao kwa kuwatumia vijana walionao.

Kupitia Msemaji wa timu hiyo, Thobias Kifaru, amesema kuwa wao ni chuo cha soka hivyo  hawana wasiwasi wowote juu ya kuondoka kwa wachezaji wao wawili kuelekea klabu kongwe za Kariakoo.

Kifaru ameeleza Mtibwa itawapasa kuandaa vijana wengine kama ilivyo sera yao ya kuwafua vijana na baadaye wanaimarika kisha kufanua vizuri kama ilivyokuwa kwa Shiza Kichuya, Mohammed Ibrahim na wengineo.

"Tutatumia vijana tulionao kutokana na utamaduni wetu wa kuwafua vijana ambao huwa wanakuja kuwa na vipaji vizuri, kuondoka kwa Dilunga na Banka kwetu wala haitupi shida kubwa" alisema.

Mtibwa imeondokewa na wachezaji Mohammed Issa Banka pamoja na Hassan Dilunga ambao wote wanacheza nafasi ya kiungo.

Banka amefanikiwa kunaswa na Yanga na kusainishwa mkataba wa miaka miwili pia Dilunga akitia kandarasi ya miaka miwili na Simba.


1 COMMENTS:

  1. HONGERA MTIBWA NI CHUO HASWA NA WALA HAMUYUMBI HATA KIDOGO KILA MWAKA

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic