July 8, 2018


Na George Mganga

Aliyekuwa mchezaji wa Stand United, Ally Ally amejiunga na KMC FC ya Kindondoni, Dar es Salaam kwa kusaini mkataba wa mwaka mmoja.

Ally amejiunga na KMC baada ya mambo kutoenda sawa katika klabu yake ya zamani kutokana na kutolipwa fedha za mshahara wake.

Beki huyo wa kati hivi karibuni aliibuka na kusema Stand kuwa anaidai mshahara wa miezi takribani mitatu na akaadhidi hataweza kuendelea kuichezea klabu hiyo.

Baada ya kuahidi kutoichezea Stand msimu ujao, beki huyo amefanikiwa kufikia mwafaka na mabosi wa KMC ambapo msimu ujao atakuwa na timu hiyo.

KMC ambayo imepanda kushiriki Ligi Kuu Kuu Bara msimu ujao imezidi kukifanyia maboresho kikosi chake ambapo imenyaka saini za wachezaji wenye uzoefu katika ligi ikiwemo kipa Juma Kaseja aliyewahi kung'ara Simba.


1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic