GOR MAHIA YAANZA VEMA ROBO FAINALI KAGAME. YAITWANGA VIPERS 2-1
Na George Mganga
Kikosi cha Gor Mahia kimeanza vema hatua ya robo fainali ya michuano ya KAGAME kwa kuibuka ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Vipers SC ya Uganda.
Gor Mahia imejipatia mabao hayo kupitia kwa Jacques Tuyisenge mnamo dakika ya 47 na Mustafa Francis katika dakika ya 43.
Bao pekee la Vipers limewekwa kimiani na Tadeo Lwanga mapema katika dakika ya 15 ya kipindi cha kwanza.
Baadaye majira ya saa 1 kamili jioni, Simba ya jijini Dar es Salaam itakuwa ina kibarua dhidi ya As Ports ya Djibout, mechi ikipigwa Uwanja wa Taifa.
0 COMMENTS:
Post a Comment